Ticker

10/recent/ticker-posts

KAMPENI YA TBS YAWAFIKIA WANAFUNZI KAHAMA

Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limeendelea na Kampeni yake katika Wilaya ya Kahama  kutoa Elimu kwa umma juu ya umuhimu wa kununua bidhaa zilizothibitishwa na TBS na jinsi gani wajasiriamali wanaweza kupata Leseni ya TBS bure bila gharama yoyote.

Kampeni hiyo ya Elimu kwa umma pia ilifanyika katika  Shule ya Msingi Malunga Mjini Kahama mapema Februari  09, 2019 huku wanafunzi zaidi ya 1000(elfu moja) wakipata elimu juu ya masuala mbalimbali yahusuyo Ubora wa Bidhaa.

Kwa upande wake Afisa Uhusiano Bi. Neema Mtemvu aliwasisitiza  wanafunzi  hao kuwa vita ya bidhaa hafifu sio ya TBS pekee bali ya kwetu sote (Wananchi na Shirika), Hivyo, tunaamini wao watakuwa mabalozi wazuri katika kuelimisha wengine na vilevile na wao kujenga tamaduni ya kuthamini ubora tangu wakiwa wadogo. Hivyo,wahakikishe wananunua bidhaa zilizothibitishwa na TBS, pale wanapotumwa madukani na masokoni.

Kampeni hiyo inaendelea tena Mkoani Mara Mara baada ya kufanyika mikoa ya Kagera, na Shinyanga.
 Pichani: Ni Afisa Uhusiano wa TBS Bi. Neema Mtemvu akiendelea kutoa elimu kwa wanafunzi wa shule ya Msingi Malunga ya Mjini Kahama Mkoani Shinyanga, namna ya kutambua bidhaa hafifu ambazo hazijathibitishwa.



from MICHUZI BLOG http://bit.ly/2SkFZbt
via

Post a Comment

0 Comments