Ticker

10/recent/ticker-posts

Marekani yatangaza vikwazo dhidi ya Warusi 38 na makampuni ya Urusi

Ikulu ya Marekani, White House imetangaza vikwazo dhidi ya Warusi 38 na makampuni, ikisema Marekani inakabiliana na kile kinachoendelea ikiwa ni mbinu za Serikali ya Urusi  za “vitendo vya kuvuruga” demokrasia nchi za Magharibi na ulimwenguni kote.

Katika muhtasari alioutoa msemaji wa White House Sarah Huckabee Sanders Ijumaa amesema Marekani bado inataka kushirikiana na Urusi

“Pia, kile tunachotaka kukiona ni serikali ya Urusi ibadilishe mwenendo wake kikamilifu. Tunataka kuendelea kuwa na mazungumzo na kufanya kazi siku za usoni kwa kujenga mahusiano mazuri,” Sanders amesema.

Vikwazo hivyo vitawekwa dhidi ya makampuni saba ya Urusi – ikiwemo Oleg Deripaska, kampuni ya aluminium ambayo ni mshirika wa karibu na Rais Vladimir Putin- na makampuni mengine 12 ambayo wanayamiliki au kuyahodhi.

Pia maafisa 17 wa serikali ya Urusi, na kampuni ya kutengeneza silaha inayomilikiwa na serikali ya Urusi na kampuni zake tanzu, benki ya Urusi, pia zitalengwa na vikwazo hivyo.