Ticker

10/recent/ticker-posts

BIG JAHMAN ANYOOSHA MAELEZO JUU YA MAHUSIANO YAKE NA SARAHA

Pamekuwa na minong’ono na ishara kuwa msanii wa bongo fleva mwenye asili ya Sweden mwanadada Saraha sasa anatoka kimapenzi na Big Jahman ambaye pia ni msanii wa bongo fleva, baada ya kuachana na producer Fundi Samweli.
Big Jahman alikanusha mbele ya Kamera ya eNewz na kusema kuwa Saraha ni zaidi ya familia kwake na wana sapotiana zaidi kwa upande wa muziki lakini hawana mahusiano yeyote ya kimapenzi na kwamba anaheshimu sana familia yake hivyo hawezi kuwa na mahusiano na Saraha.
Big Jahman
Hata hivyo Big amesema watu wanajiongeza kuwa yeye na Saraha wanamahusiano kwa kuwa ni mwanamke na yeye ni mwanaume lakini wanasapotiana tu kimuziki na si vinginevyo.

Mbali na hilo, jana feb 10, Fid Q alimtangaza rasmi Big Jahman kama msanii wa kwanza kwenye label yake ya cheusi Dawa. Utambulisho wake umeenda sambamba na kuachia kazi yake iitwayo Mabundi aliyowashirikisha Fid mwenyewe na Saraha.