Ticker

10/recent/ticker-posts

Hawa ndio Mastaa Bongo wenye mashabiki wengi instagram

Mastaa Bongo wenye mashabiki wengi instagram
Ni staa wa Bongo Fleva anayebamba na Ngoma ya  Make Me Sing. Diamond
anashikilia usukani kati ya  mastaa wa Bongo wenye mashabiki wengi ambao
ni zaidi ya milioni mbili (2,046,428).

Ni staa wa filamu Bongo. Wema Sepetu anashikilia nafasi ya pili akiwa na wafuasi zaidi ya  milioni moja na nusu (1,594,606).

Ni mtangazaji maarufu nchini akimiliki pia studio yake binafsi ya kurushia  matangazo. Millard ambaye amejizolea  umaarufu kwenye mitandao na redio ana mashabiki zaidi ya milioni moja na nusu (1,577,345).

Mwanamitindo na Muigizaji, Jokate Mwegelo anasimama katika nafasiya nne akiwa na mashabiki
zaidi ya milioni moja na laki nne (1,497,197). Jokate
kwa sasa anamiliki lebo yake ya Kidoti inayojishusisha
na bidhaa za urembo.

Unaweza kumuita Wolper  Gambe. Mwanadada huyu ambaye ni mkali katika
tasnia ya uigizaji Bongo, ana mashabiki zaidi ya  milioni moja na laki nne
(1,476,933).

Vee Money kama anavyojulikana katika  tasnia ya Muziki wa Bongo Fleva, naye ni miongoni
mwa mastaa wenye  mashabiki wengi akiwa na mashabiki zaidi ya milioni moja na laki nne (1,401,187).

SHILOLE (1.3M)
Ni staa wa Muziki wa Bongo Fleva pamoja na filamu. Shilole ama
Shishi amejizolea umaarufu kwenye nyimbo kama  Malele na Namchukua, ana
mashabiki wengi kwenye  mitandao ambao ni zaidi ya milioni moja na laki tatu. (1,377,428)
DIAMOND (2M) 
WEMA (1.5M) 
MILLARD (1.5M) 
JOKATE (1.4M)
WOLPER (1.4M)
 VANESSA (1.4M)