Ticker

10/recent/ticker-posts

Jinsi ya kutengeneza mahusiano yaliyovunjika

Image result for mapenzi imageMahusiano yoyote huwa ni rahisi sana kuvunjika endapo mmoja wenu  akimkwaza mwenzake,kutokuwa na maelewanao  au kwa sababu zilizo nje ya uwezo wao. Huwa ni kazi ngumu sana kurekebisha mahusiano yaliovunjika mpaka yarudi katika hali ile iliokua zamani kwa kuwa doa tayari limeshaingia kwenye mahusiano. Japo kuwa mahusiano huwa yanatofautiana  baina ya wahusika mbali mbali ila katika njia za kuyarekebisha ili yakae huwa zinalingana. Baadhi ya vitu vinavyoweza saidia kurekebisha mahusiano yaliovunjika ni;

Elewa sababu ya kuachana
Kabla haujaanza tafuta suluisho la tatizo, elewa kwa kina uzito wa tatizo lenyewe kisha ndio uanzie hapo. Bila kuelewa mzizi au chanzo cha tatitzo huwa inawia vigumu kurekebisha kwa kuwa  hicho chanzo kinaweza kuwa kilitokea wakati uliopita na sasa hakipo ama bado kinaendelewa kuwepo kwa hiyo hatua labda zinabidi zichukuliwe ili kukabiliana nalo. Likishajulikana tatizo inakua rahisi sana kurekebisha na pia inawapa mwanya kwa wapenzi kutambua mapungufu yao na kujirekebisha  kwa ufasaha.

Msamaha ni muhimu
Mkisha fanikiwa kudadavua chanzo cha kuachana, kinachofwata nikusameheana na kushahau yaliopita ili muweze tengeneza mwanzo mzuri wenye mafanikio. Itakulazimu uelewe kwa nini mwenza wako alifanya kosa kama lile ili huko mbeleni lisijirudia maana inawezekana alikua anakosa kitu toka kwako ndio maana akajikuta anaenda fanya kosa kama hilo la labda kutembea nje ya mahusiano. Kuungana kwenu tena kunaweza fungua ukurasa wa maisha mapya tena yenye upendo mkubwa kwa kuwa mlikua wazi baina yenu kipi kina mkera mwenzako na kasha mkasameheana.

Kujitoa upya kwa mwenzako
Mkisharudi kwenye mahusiano, ni vyema ukajitoa upya kwa mwenzako zaidi ya mwanzo (renew the commitment), hii itasaidia kumuonyesha mwenzako kwamba unajutia kwa kile ulichokifanya na upo tayari kujirekebisha kwa hali na mali na pia utaendelea kumjali na kumuheshimu. Kuwa na msimamo katika kujitoa kwako kwake ni muhimu sana maana ukijitoa sa hivi halafu ukaja badilika baade tatizo lile lie litajirudia na mtarudi kule kule mlipotokea kwenye matatizo.

Badilisha mwenendo
Huwa ni ngumu sana kumbadilisha mtu kwenye mahusiano,kuna  baadhi ya vitu mnaweza kuwa na mtazamo tofauti. Ukiona hali kama hii ipo, basi haina budi kujibadilisha mwenyewe yani kujaribu kumwelewa mwenza wako na kisha tumia njia mbadala ya kujaribu kumweka sawa. Kuna watu wengine huwa wanajifunza kwa mifano, matendo na wala si maneno. Jaribu kumuonyesha mifano dhahiri ya aina mbali mbali kuhusu jambo mpaka atakapojirekebisha.

Mawasiliano baina yenu
Nikizungumzia mawasiliano simaanishi haya ya simu za mkononi au barua pepe bali namaanisha ya kuwa mazungumzo kati yenu ndio yatakua ufunguo mkubwa wa ushuluishi wa matatizo yatakayowatokea. Mahusiano mengi yanayovunjika utakuta mengine ni kwa sababu ya sababu ndogo sana ambazo zilikua zinazungumzika ila kutokana na kupuuzia ndio mambo yakaendelea kuwa makubwa zaidi.  Hakikisheni mawasiliano yenu yawe chanya yani mnaelezana ukweli, kama mwenzako kakukwaza kisha mnatazama mtumie njia gani za kuweza kutatua tatizo hilo

The post Jinsi ya kutengeneza mahusiano yaliyovunjika appeared first on Vibe Magazine TZ Tanzania.
Vibe Magazine TZ