Ticker

10/recent/ticker-posts

WAONE HAPA MASTAA WA BONGO FLAVA WALIOPOTEA NA KURUDI KWA KISHINDO


Muziki wa Bongo Flava unafanya vizuri kwa sasa, unashika nafasi ya tatu kwa Afrika baada ya Nigeria na Afrika Kusini.
Kwa jinsi ushindani ulivyokuwa mkubwa kwa sasa kwenye industry ya muziki wa Bongo Flava ni ngumu kwa msanii kukaa muda mrefu bila ya kuachia wimbo mpya. Kuna baadhi ya wasanii wachache waliopata bahati ya kukaa kimya kwa muda mrefu bila ya kuachia wimbo lakini waliporudi wakakuta nafasi zao bado zipo wazi.
AlikibaHitmaker wa nyimbo kibao; ‘Cinderella’, ‘Mapenzi Yanarun Dunia’, n.k. aliweza kukaa takribani kwa muda wa miaka mitatu bila ya kuachia wimbo wake wowote, lakini alikuwa anashirikishwa kwenye nyimbo za wasanii wengine.
Kukaa kimya kwa Alikiba kuliibua hisia tofauti kwa mashabiki wake huku wakishindwa kuvumilia fedheha kutoka kwa mashabiki wa Diamond Platnumz. Haikuwa rahisi kwa team Kiba kukubaliana na matokeo, lakini ndiyo hali halisi iliyokuwepo kwa kipindi hiko.
‘Kimya kingi huwa kina kishindo’, baada ya kimya cha muda mrefu Alikiba akawafurahisha mashabiki wake waliomsubiri kwa muda mrefu kwa kuachia ‘Mwana DSM’. Ilikuwa ni kama neema, baada ya kuachia wimbo huo kafanikiwa kupata tuzo tano za KTMA.
Tangu hapo mashabiki wa Aliliba wamepata nguvu ya kupambana tena na mashabiki wa Diamond.
Q Chief

Q Chief ni miongoni mwa wasanii wa Bongo wenye uwezo mkubwa wa kuimba na kipaji cha ukweli.
‘Si Ulinikataa’, ‘Uhali Gani’, ‘Namtafuta’, ‘Tutaonana Wabaya’ ni miongoni mwa nyimbo za Q Chief aka Q Chilla ambazo hazitasahaulika. Alikaa muda mrefu bila ya kutoa wimbo huku akihusishwa kuingia kwenye matumizi ya madawa ya kulevya lakini ameweza kupambana na kutoka huko.
Watu walipata mshangao walipoisikia ‘For You’, hakika ilikuwa ni furaha kwa mashabiki wa Bongo Fleava kwa ujumla kwa sababu kuna vitu vilikuwa vinakosekana wakati Q Chilla yupo nje ya industry ya muziki.
Tangu alipoachia ‘For You’ mwaka jana, Q Chilla ameendelea kuachia nyimbo ambazo zinaendelea kufanya vizuri kwenye media mpaka sasa ‘Power Of Love’ na ‘Mkungu Wa Ndizi’.
Lady Jaydee

Moja kati ya wasanii wenye mafankio makubwa na waliotengeneza heshima kwenye muziki wa Bongo Fleva hutoacha kumtaja Lady Jaydee.
Jide anajulikana kama; Anakonda, Commando na majina mengi anahit kibao zilizowahi kufanya vizuri ‘Siwema’, ‘Siku Hazigandi’, ‘Machozi’, n.k. Tangu alipoachia wimbo wa ‘Give Me Love’ aliomshirikisha Mazet na DJ Maphorisa, Jide hajaweza kutoa wimbo mwingine mpaka alipoachia wimbo wa ‘Ndi ndi ndi’ wiki iliyopita.
Mashabiki wa Jide walikuwa hawajaelewa nini kitakachotokea baada ya kuona post za ‘Naamka Tena’ zikienea kila siku hadi zilipotimia siku 30. Haikujulikana kama nini kingeweza kutokea, walipata mshangao siku ilipofika na kuisikia ‘Ndi ndi ndi’ ikipenya kwenye masikio yao.
Kweli Komando Jide kaamka tena, lakini anapaswa kujua mashabiki wake waliteseka sana kwa kipindi ambacho alikuwa kimya. Nadhani kwa hii zawadi ya wimbo aliyowapa watakuwa wameshasahau machungu waliyoyapata mwanzo.