Ticker

10/recent/ticker-posts

HIVI NDIVYO VITU SITA MUHIMU SANA VYA KUJIFUNZA KABLA HUJAINGIA KATIKA MAPENZI,SOMA ZAIDI HAPA LIVE.

Kama unatarajia kuingia katika uhusiano wa kimapenzi kwa matarajio ya kufanikiwa kuyamudu basi kuna vitu vya muhimu sana ambavyo lazima ujifunze kabla ya kuanza uhusiano mpya.Hivi ndivyo vitu sita vya kufanya kabla ya kuingia katika mahusiano.

1.Kubali masuruhisho/mapatano:
Uhusiano ni kati ya watu wawili,kwa hiyo siyo kila mara kupata kile unachokihitaji au mambo yaende sawa kama vile unavyotaka mda wote.Lazima ujifunze wakati mwingine kuacha mambo yaende tu hata kama wakati mwingine hutaki ili naye mpenzi wako afanye vitu anavyovitaka yeye kama yeye.Wakati mwingine mpe mpenzi wako nafasi ya kufanya mambo anayoyataka.

2.Msamaha:Mpenzi wako mara nyingi atajikuta anafanya mambo ambayo huyataki au huyapendi au mambo ambayo yataharibu hisia zako,hii haimaanishi kuwa lazima umkasirikie mpenzi wako au umjengee hisia za visasi.Katika mahusiano ya kimapenzi wote wawili lazima muwe tayari kusameheana nyinnyi wote ni binadamu lazima muwe na uwezo wa kusameheana kwa kuwa wote mnaweza kufanya makosa wakati wowote.

3. Omba msamaha: Kuna faida kubwa na umuhimu mkubwa sana wa kuomba msamaha,lazima ujue na uwe makini sana na swala la kumuomba msamaha mpenzi wako unapokuwa umemkosea.Lazima uwe na uwezo mkubwa wa kutambua ni wakati gani umemuumiza mpenzi wako na uwe mwepesi zaidi kuomba msamaha kwa moyo wote.Kuwa mwepesi zaidi kukubali makosa yako na uwe mwepesi kuyaombea msamaha na kujifunza kutoyarudia mara kwa mara.

4.Zungumza kwa upole:Wakati watu wawili wanapopendana na kuanza safari ya mapenzi,ni muhimu sana kushughulikia swala la mawasiliano baina yao na swala hili ni gumu sana kama mmojawao atashindwa kujibu au kuwasilisha hoja zake kwa mwenzake kwa upole,lazima uwe mbunifu kila siku kwa kutafuta maneno mazuri ya kuwasiliana na mpenzi wako kwa upole na umakini wa hali ya juu sana maneno ni siraha kubwa sana kwa mpenzi wako itumie vizuri kwa upole utaona matokeo yake.

 5.Jifunze kusikiliza: Huwezi kuhimili usiano wa kimapenzi kama mpenzi wako hapenzi kuongea na wewe au hujisikii/hajisikii kuongea na wewe.Ili uweze Kufanya mambo yako yaende vizuri lazima uwe tayari kuwa msikilizaji lazima uwe mtu ambaye mpenzi wako akipata matatizo akukimbilie wewe,hata kama tatizo liwe la siri kiasi gani au gumu namna gani.

6.Jitambue na kujikubali:Kama hujikubali wewe mwenyewe na hauna furaha na jinsi ulivyo,haishangazi kuona kuwa na wewe pia hutamkubali pia mpenzi wako pia.Hakikisha ni kitu gani kinakufanya upende usipende kitu fulani,hobi zako vitu ambavyo unapenda kufanya katika maisha yako, michezo unayoipenda n.k.Mambo kama hayo yatakufanya uchague mpenzi sahihi unayempenda kutokana na sifa zako na tabia unazozipenda katika maisha yako.

Post a Comment

0 Comments