Ticker

10/recent/ticker-posts

RAIS KAGAME AFUNGUKA MAZITO KUHUSU RAIS MAGUFULI.. SOMA HAPA ALICHOSEMA

April 6 2016 Rais John Magufuli wa Tanzania aliungana na Rais Paul Kagame wa Rwanda katika ufunguzi wa daraja la kimataifa mpakani mwa Tanzania na Rwanda na wakafungua pia Ofisi ya pamoja itakayokua inadili na ishu za uhamiaji upande wa Tanzania na Rwanda kwenye huo mpaka.
Kwenye nukuu zilizotolewa na ofisi ya Rais Rwanda kutoka kwa Rais Kagame ambaye aliyasema haya baada ya Rais Magufuli kuondoka Rwanda, ni pamoja na hii >>> ‘Kwa uongozi mpya, sasa Rwanda na Tanzania watafurahia uhusiano mzuri na kila tatizo litatuliwa‘
Hii ni kauli ambayo Rais Kagame aliisema wakati wa kumbukumbu ya mauaji ya kimbari Rwanda na aliyazungumza haya mbele ya maelfu ya Wananchi waliokusanyika kwenye uwanja wa mpira Amahoro Kigali Rwanda ambapo pia Rais Kagame alimshukuru Rais Magufuli kwa kuitembelea Rwanda kupitia page yake ya Twitter.
Rais Kagame alisisitiza pia kwamba ‘Wote wanaojaribu kuliangamiza taifa letu ikiwemo na wale wanaowatumia nchi ambazo ni jirani zetu kamwe hawatoweza kufanikiwa‘