Ticker

10/recent/ticker-posts

Jokate Aumizwa na Maneno ya ALI KIBA Kuwa Wao ni Marafiki Tu...Ampiga Kijembe Kwa Kutumia Wimbo wa Lady Jay Dee

Huenda maneno ya Alikiba kwenye E-News yameanza kumuumiza Jokate.

Mwanzoni Jokate na Alikiba walionekana kuwa karibu sana lakini siku za hivi karibuni kila mmoja ameonekana kuwa peke yake.

Jokate ameonekana kuumizwa na maneno ya Alikiba aliyojibu kwenye kipindi cha E-News, kinachoruka kupitia EATV. Mrembo huyo ameamua kupost kwenye akaunti yake ya Instagram na kuweka maneno yanayozidi kuzua maswali mengi juu ya mahusiano yake na muimbaji huyo.

Jokate aliweka pichaya kwanza na kuandika, “Mpende akupendaye. Asiyekupenda achana nae!!!


Alikuja kupost picha ya pili na kuandika maneno aliyocopy baadhi ya mistari ya kwenye nyimbo ya Lady Jaydee ‘Ndindindi’. “Niliwezaje kutoa vyote ili hali wewe ulininyima vyote, kama ni jipu lilivimba zaidi. Nikasahau chizi huwa haponi kama chozi mvuani. Hatimaye kumekucha na milembe nimekushusha. Na geti likifungwa naondoka.”

Je Paradise pamevurugika?