Ticker

10/recent/ticker-posts

ANGALIA FEDHEHA YA FUMANIZI HILI LA MZEE MTU MZIMA


HII ni ni fedheha! Mzee Mbonde, mkazi wa Kimara jijini Dar, anadaiwa kutelekeza familia na kwenda kuishi na mwanamke mwingine gesti kisha kufumwa laivu na mkewe, Herieth Mngodo.

Mzee Mbonde baada ya kufumwa live na mkewe akiwa gesti na mwanamke mwingine.
Tukio hilo lililokusanya kadamnasi ya mjini, lilijiri wikiendi iliyopita katika gesti iitwayo New Samri, Manzese jijini Dar ikiwa ni sehemu ya kazi nyingine nzuri ya Oparesheni Fichua Maovu (OFM) ya Global Publishers.
SARAKASI ZA NDOA
Kwa mujibu wa chanzo chetu, Mzee Mbonde ambaye aliwahi kuwa Diwani wa Kata ya Sinza- C, Dar, alidaiwa kuitelekeza familia yake (mke na watoto watatu) na kuishi na mwanamke mwingine katika gesti hiyo tangu mwishoni mwa mwaka jana.
Mke wa Mzee Mbonde akitema cheche baada ya kumfumania mumewe.
Chanzo hicho kilizidi kudai kuwa, Mzee Mbonde alioana na mkewe huyo mwaka 1984, bomani na ilikuwa ni ndoa ya mke mmoja.
Kilidai, mwishoni mwa mwaka jana mzee huyo alianza, ‘kuchepuka kutoka njia kuu’ na kuanzisha uhusiano na mwanamke wa nje kisha kwenda kujichimbia naye kwenye gesti hiyo.
UMBEYA WAMFIKIA MKEWE
“Mjini watu watakunyima ugali siyo maneno, kuna watu walimtonya mama Herieth kuwa mumewe anaishi katika gesti hiyo ndipo alipovaa kininja na kwenda kufanya utafiti, akabaini kuwa ni kweli na kuwajuza OFM,” kilisema chanzo hicho.
OFM MZIGONI
Kikosi kazi cha OFM, baada ya kumegewa mchapo huo, kilitinga katika gesti hiyo na kupanga chumba ambacho kilikuwa kinatazamana na chumba cha diwani huyo mstaafu kwa siku tatu kuchunguza kama kweli kigogo huyo anaishi na mwanamke mwingine, ‘results’ zikaonesha ni kweli.
MUVI LILIVYOANZA
Baada ya OFM kumpa majibu mke huyo wa diwani mstaafu, alikusanya nguo zote za mumewe akaambatana na mwanaye wa kike kwenda kwenye gesti hiyo kumkabidhi.
“Sitaki ugomvi na mume wangu, kaamua kunitelekeza na familia, dawa yake ni kumpelekea hizi nguo zake ili aendelee kuishi na huyo mwanamke wake hukohuko,” alisema mama huyo.
FUMANIZI KABANG!
Huku makamanda wa OFM wakifuatilia kwa karibu na kunasa picha hatua kwa hatua, walimshuhudia mama huyo akizama na Bajaj katika gesti hiyo, akagonga katika chumba cha mzee huyo, alipofungua tu, alimnyunyizia mumewe pilipili machoni na kuanza kumtupia nguo zake.
Timbwili zito liliibuka, mke alianza kumzaba makofi mumewe, ndani ya muda mfupi watu kibao wakajaa nje na ndani ya gesti hiyo kumshuhudia mzee huyo akiangua kilio, hali iliyowashtua wateja wengine waliopanga katika gesti hiyo.
MFUMANIWAJI ATOKA NDUKI
Wakati timbwili likiendelea, mwanamke aliyefumaniwa alifanikiwa kupata mwanya na kutokomea kusikojulikana hivyo msala ukabaki kwa diwani huyo mstaafu.
Mke huyo, baada ya kutekeleza matakwa yake (fumanizi), naye aliondoka eneo hilo na mwanaye kuelekea nyumbani kwao na kumuacha mumewe akiwa hoi kwa maumivu ya pilipili machoni kwani yalishaanza kuvimba.

CREDIT:GLOBAL PUBLISHERS