Ticker

10/recent/ticker-posts

WASKIE MASTAA WANAVYOZUNGUMZIA UCHAGUZI MKUU TANZANIA 2015..

Na Gladness Mallya
IKIWA kesho Jumapili ndiyo siku ya uchaguzi mkuu ambapo Watanzania wataamua nani awe rais wao, mastaa mbalimbali wamezungumza na Risasi Jumamosi kueleza walivyojiandaa na uchaguzi huu ambao unaonekana kuwa na changamoto nyingi kuliko nyingine zote zilizopita:
AMANDA POSHI
Uchaguzi wa mwaka huu ni wa tofauti sana na zilizopita maana Watanzania wengi wana mihemko na hamu sana kutokana na ushindani mzito uliopo, nimejiandaa vyema kikubwa tuombe uhai. Kura yangu ni kwa Magufuli. Niwahusie Watanzania kwamba wazingatie sheria zote za uchaguzi zilizowekwa ili kuepuka kuharibu kura zao.
HALIMA YAHYA ‘DAVINA’
Uchaguzi huu umejaa changamoto sana, kuna upinzani mkali kuliko miaka yote, cha muhimu naomba amani itawale jamani tukubaliane na matokeo yoyote yatakayotokea. Tukumbuke Tanzania ni nchi yenye amani hivyo tusivurugwe na itikadi za vyama tukasahau kwamba amani ni kitu muhimu kuliko kitu kingine chochote. Mtanzania nenda kapige kura yako rudi nyumbani.

YUSUPH MLELA
Mimi nimejiandaa vizuri lazima nipige kura kwa sababu ni haki yangu ya msingi, uchaguzi huu umekuwa wa ushindani sana kwa sababu vijana wameamka sana tofauti na miaka ya nyuma tegemeo kubwa ni kuona mabadiliko. Kikubwa ninachomuomba Mungu ni amani pia Watanzania tulizingatie hilo kwani tukiivuruga hatuwezi kuipata tena.
KULWA KIKUMBA ‘DUDE’
Uchaguzi wa mwaka huu una changamoto nyingi ni muhimu watu wakasikiliza sera zaidi maana watu wengi hasa vijana wameibuka kuwa mashabiki wa vyama bila kujua sera za vyama husika, yote kwa yote uchaguzi ni mgumu sana na utakuwa na matokeo ya kushangaza mno. Jamani tumuombe Mungu atupitishe salama kwenye hili maana wapo wanaofuata mkumbo wanaoweza kufanya vurugu zisizokuwa na msingi.