Ticker

10/recent/ticker-posts

MPANGO WA KUMUUA DR. SLAA: MLINZI WAKE ALIPUKA....ADAI CHADEMA NI MAGAIDI......ASIMULIA JINSI ALIVYOTESWA NA KUPOTEZA NGUVU ZA KIUME

Siku chache kupita baada ya Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mabere Marando kufichua njama za Mlinzi wa Katibu Mkuu wa Chama hicho Wilbroad Slaa, bwana Khalid Kangezi kupanga mipango ya kumuua  katibu huyo huku akishirikiana na Vigogo wa Chama Mapinduzi CCM pamoja na Mkuu wa Usalama wa Taifa Mkoa wa Kinondoni,naye Mlinzi huyo ameibuka  na   kufichua siri nzito ndani ya Chama hicho kikuu cha upinzani nchini..
 
Akifichua siri hiyo leo  mchana  Jijini Dar es Salaam mbele ya Waandishi wa habari, Kangezi amesema amesikitishwa  sana na madai ya uongo yanayoenezwa na viongozi wa CHADEMA  huku wakificha ukweli wa Mambo kwani ukweli wa yeye kuzushiwa uongo huo unatokana na kuwa na mahusiano na Mke wa Dr. Slaa .
 
“Nawashangaa sana hawa Viongozi wa Chadema wanaosema mimi ni nimehusika katika mipango ya kumuua Dr. Slaa. Wanaficha ukweli tu kwani sababu  ya kuzushiwa uongo  huu inatokana na mimi kuwa na mahusiano mabaya na Mke wa Slaa...

"Nilipoenda kumwabia Slaa, alisema niende nikamalizane na  mke wake lakini ukweli ni kuwa mambo hayakwenda vizuri, mke  wake  hakunielewa , ndipo  Slaa akapeleka  sakata  hilo  kwenye uongozi wa juu” amesema kagenzi  na  kuongeza:

"Baada ya Dr. Slaa kupeleka ugomvi huo kwenye ngazi za juu,juzi  wakati  naenda  ofisini nilikamatwa na kupelekwa  chumba cha  mateso  kinacho  milikiwa  na  Chama  hicho"
  
 Mlinzi Kagenzi akionyesha mateso aliyofanyiwa na  Makada wa Chadema
Bwana Kagenzi ameendeleo kusema kuwa hata madai wanayodai kwamba anauhusiano wa karibu na usalama wa Taifa pamoja na Vigogo wa CCM   ni ya uongo.
 
“Jamani hivi inaingia akilini kweli mimi leo na maisha yangu haya niwe na uhusiano na watu wa usalama na CCM,huu ni uongo wa hali ya juu na wanataka kunichafua kwa jamii tena niseme ukweli chama hiki kinataka kuficha ukweli juu ya mambo waliyonitendea.
 
“Mimi nimekuwa mlinzi wa Dr. slaa kwa muda wa miaka mingi sana ,tena nilikuwa nampikia na kumtengea hadi chai ya kunywa eti leo niambiwe naandaa mipango ya kumuua ? Huo ni unafiki” amesema Kagenzi
  
Akionyesha Vidonda
Mlinzi huyo ameenda  mbali  zaidi  na  kufichua  mipango ya kigaidi inayofanywa na Chadema huku akisema wameandaa ofisi  ya utesaji.
 
“Chama ambacho kinandoto ya kuchukua nchi leo kinaandaa mipango ya mauaji na utesaji kama walivyonifanyia .
  
"Waliniteka na kunifungia kwenye chumba cha mateso  wanachomiliki wao, wamenichoma visu na kuniweka kwenye Mashine  ya umeme bila kosa lolote,eti wakinishinikiza  nitaje wanaonituma. Jamani nawaambia  ukweli  na  watanzania  wajue, situmwi  na  mtu  yeyote” .
 
Aidha, Kagenzi amekitupia lawama chama hicho na  kusema  kuwa  mateso waliyomtesa yamemfanya apoteze nguvu za kiume .
  
Kuhusu kuingiziwa Milioni saba kwenye simu yake na watu wa Usalama wa Taifa, Kagenzi amesema hizo ni taarifa za uongo  kwani hata simu yake haina salio  na haijawahi kupokea pesa hizo. 
 
Kagenzi  amehitimsha  kwa  kusema  kuwa baada  ya  mahojiano  na  jeshi  la  polisi  sasa  anajipanga  kufungua  kesi  mahakamani  ili  kuwashitaki  CHADEMA  kwa  mateso  waliyompa.