Ticker

10/recent/ticker-posts

SOMA HAPA ALICHOANDIKA HEMEDY PHD KUHUSU MSANII WA TANZANIA ALIESEMA HAFANYI TENA COLLABO NA WABONGO.

Screen Shot 2014-11-10 at 11.03.32 AMMwigizaji/Mwimbaji Hemedy PHD ni miongoni mwa mastaa wa Tanzania ambao hutumia sehemu ya muda wao pia kuandika kwenye mitandao ya kijamii yake ya moyoni ama kuwafikishia taarifa mashabiki wake.
November 10 2014 Hemedy aliandika tweet ikisema >>> ‘Mtu anasema hategemei kufanya collabo na msanii wa bongo ikiwa ngoma zake zote kabebwa na collabo, fikiri kabla ya kuzungumza‘
Hemedy ameandika tweet hii siku kadhaa baada ya msanii Shetta kusema kwa sasa hafikirii kufanya collabo na Wasanii wa Tanzania bali anafanya mpango wa kujipenyeza kimataifa zaidi akisema ‘nimefanya collabo nyingi na Wasanii wa Tanzania ndio maana siko tayari kufanya tena hivyo nikawa nawaza mawili, nifanye collabo na msanii wa kimataifa au kutoa wimbo peke yangu?