Ticker

10/recent/ticker-posts

ANGALIA HAYA YALIYOMPATA MSANII NYOTA NDOGO..NA WEWE YANAKUHUSU PIA

nyotandogoinside_20140405
Nyota Ndogo amesema ameamka asubuhi na kuvalishwa pete hiyo, anamshukuru Mungu kwa hilo kwani mpenzi wake hampendi yeye peke yake bali anawapenda na watoto wake wawili na anatarajia ndoa yake itakuwa ya kawaida ambayo watu wachache watakaopata nafasi ya kuhudhuria ikiwemo ndugu na marafiki wachache.

Wedding
Uchumba, ndoa zote ni taarifa nzuri kuzisikia. Una taarifa kuhusu Nyota Ndogo?
Mwanamuziki huyo kaingia kwenye orodha ya mastaa wanaoelekea kubadilisha status zao baada ya kuvalishwa pete ya uchumba.

Nyota Ndogo ambaye jina lake halisi ni Mwanaisha Abdalla amevalishwa pete hiyo na Henning Neilsen raia wa Denmark baada ya kuwa kwenye uhusiano kwa zaidi ya miezi tisa.