Ticker

10/recent/ticker-posts

Sugu alalamika DC Benno Malisa Kukwamisha Maandamano CHADEMA Mbeya

 Sugu Amshukia DC Kuhujumu Maandamano Chadema

Mbunge wa zamani wa Mbeya Mjini kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ ametumia takriban dakika tano za hotuba yake, akidokeza kile alichokiita figisu za za kisiasa kuzuia mkutano wa hadhara wa chama hicho, huku akimtaja Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Benno Malisa kuwa mmoja wa waliohusika.

Hata hivyo, alipotafutwa Dc Malisa kuzungumzia kauli hiyo alisema ameisikia na anasubiri taarifa rasmi, huku akifafanua kuwa maandamano hayo yaliruhusiwa na Rais Samia Suluhu Hassan na ndiyo maana hakuna aliyezuiwa kushiriki.

 Alisema hata Naibu Waziri Mkuu, Dk Dotto Biteko kugongana nao kwenye msafara, alitumia busara katika kuwapisha njiani kutekeleza ‘4RS’ ya Rais Samia, akiahidi baada ya kupata taarifa rasmi ataielezea zaidi.

“Nimesikia ila sijapata taarifa rasmi, lakini maandamano yalifanyika na hakuna aliyezuiwa kwa sababu tayari walishapewa kibali na Rais Samia, hivyo hayo mengine tusubiri,” alisema Malisa.


Post a Comment

0 Comments