Ticker

10/recent/ticker-posts

Soma alichoandika Kijah Yunus wa Clouds 360 kuhusu Lowassa

 

Anaandika Mtangazaji Maarufu wa Kipindi ca Clouds 360 cha Clouds Tv Bi Kijakazi Yunus….Endelea

….Ikiwa leo ndio siku yetu ya mwisho kukuona japo si kwa sura ila kuona Jeneza lako, siku ambayo unakwenda kupumzishwa katika nyumba yako ya milele hapa kwenye eneo la makazi yako Ngarash wilayani Monduli Mkoani Arusha, naomba na mimi niseme japo moja tu kuhusu wewe Hayati Edward Ngoyai Lowassa. 


Kwa wasiofahamu, nilipata nafasi ya kuwa karibu na Mh. Edward Lowassa na kwangu alikuwa Baba na Mlezi. Tulikutana na kuzungumza mara nyingi lakini nakumbuka zaidi siku ambayo alihitimisha ziara yake ya kutafuta wadhamini katika Maeneo mbalimbali ya Tanzania, siku alipohitimisha pale Zanzibar na kurejea Dar Es Salaam akiwa ofisini kwake Masaki alinipigia simu na kunitaka niende ofisini hapo ambapo kiukweli sikuwahi kuifahamu ofisi hiyo bali niliifahamu ile ya Mikocheni tu na ndipo nilimtembelea mara kwa mara. 

Baada ya kumwambia siifahamu, alishangaa hujawahi kuja hapa? Kisha akanielekeza mpaka nikafika, nilipoonana nae tu alisema maneno haya, “Kijakazi umefika? Nilitaka nikuone tu unichekeshe maana sijakuona siku nyingi” tukaingia ofisini ambapo tulizungumza kwa muda usiozidi dakika 15, alitaka kujua naendeleaje, akanieleza jinsi kazi ya kutafuta wadhamini ilivyokuwa lakini mwisho akaniambia, “naenda kupumzika nilitaka unione Binti yangu maana nitakuwa busy tunaweza kukosa muda wa kuonana. Mara kwa mara tulionana na hakika nilikuwa nampa story za kufurahisha na kumchekesha kama alivyotangulia kusema alitaka nimchekeshe. Nalikumbuka hili na kuendelea kuthamini kutokana na jinsi ambavyo tunafahamu alivyokuwa na watu wengi lakini katika wachache na mimi alinikumbuka siku ile na kuamua nimuone, nimejawa na shukrani sana na zaidi namshukuru Mungu kwa kupata nafasi ya kukusindikiza katika safari yako ya mwisho 🙏🏾

Kingine ambacho nilikuwa nakifurahia zaidi ni tabia yake ya kupenda kuniita jina langu kamili, Kijakazi na alikuwa anasema acha hao wakuite Kijah mimi napenda kukuita Kijakazi. 

Ninayo mengi ya kukumbuka kuhusu wewe Baba ila leo nimeona nikumbuke hilo tu. Pumzika Baba, nitakukumbuka daima, nitakulilia na nitaendelea kukuombea kama ninavyowaombea wazazi wangu na watu wangu wengine wa karibu kutokana na mchango wako mkubwa katika maisha yangu. RIP Dad 💔🙏🏾Post a Comment

0 Comments