Ticker

10/recent/ticker-posts

RC Senyamule afanya ziara ya kusikiliza kero za Wananchi Wilayani Kongwa - Dodoma,Spika Mstaafu Ndugai naye atia neno

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule amefanya Mkutano wa hadhara wa kuongea, kusikiliza na kutatua kero mbalimbali za wakazi na Wananchi wa Kata ya Mlali Wilayani kongwa.

Mkutano huo umefanyika Februari 27,2024 katika Viwanja vya ccm vya Kata hiyo ambapo Mhe. Senyamule ameweka bayana miradi ya maendeleo iliyotekelezwa katika Kata hiyo ikiwa ni pamoja na ujenzi wa Shule Mpya ya Ihanda umoja Sekondari, ujenzi madarasa 4 ya Shule ya Sekondari Mlali, ujenzi wa Barabara ya Mlali- Pembamoto kwa kiwango cha changarawe yenye jumla ya garama za kiasi cha fedha zaidi ya Shilingi Millioni 787.

Akizungumza katika Mkutano huo Mbunge wa Jimbo la Kongwa na Spika mstaafu wa Bunge la Tanzania Mhe. Job Ndugai, amewataka wananchi wa Kata hiyo kutunza ardhi na kuacha kuuza hovyo ardhi ya Kijiji cha Mlali Ili kuruhusu miradi mingine kupelekwa katika Kijiji hicho kutokana na uwepo wa maeneo makubwa ya ardhi.

"Ardhi tuliyonayo haiongezeki licha ya kuwa tunazidi kuongezeka inapaswa tuitunze, ardhi ya Kijiji ni ardhi ya umma ni ya matumizi ya Kijiji serikali ya Kijiji hampaswi kuitoa/ kuigawa Bure kwasababu kwa kadri mnavyoongezeka mtahitaji huduma zaidi ambazo zitatakiwa kujengwa katika ardhi hii, juzi nimeskia mmegawa hekari 30 kwa muwekezaji nimesikitika sana kwahiyo niwaombe msiendelee kugawa bure vinginevyo anayehitaji afate taratibu na alipie fedha na sio Bure," Ameeleza Ndugai

Kwa Upande Wake Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe. Mayeka Simon, Amesema kwa kushirikiana na Wakala wa Misitu (TFS ) Wilaya wanampango wa kuwawezesha wananchi kiuchumi kwa kuanzisha vikundi vya ufugaji nyuki ambapo hadi sasa wanakamilisha taratibu za kugawa mizinga 40 kwa vikundi hivyo Ili vianze kazi ya uzalishaji wa asali na kujipatia vipato vitakavyo kidhi mahitaji yao mbalimbali.

Post a Comment

0 Comments