Ticker

10/recent/ticker-posts

Katibu Mkuu wa CWT Aliyekataa UTEUZI Asimamishwa

 

BUNDI ameendelea kukiandama Chama cha Walimu Tanzania (CWT) baada ya Baraza la Kuu la chama hicho kumsimamisha ukatibu mkuu Japhet Maganga. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).


Maganga amekumbana na panga hilo ikiwa ni siku chache zimepita baada ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam ambaye ni mwajiri wake, kumfukuza kazi.

Aidha, wakati hayo yakijiri pia imeelezwa kuwa viongozi 10 akiwamo Maganga walikatwa na Jeshi la Polisi mkoani Dodoma jana Ijumaa kutokana na tuhuma za kufanya vurugu kwenye mkutano wa chama hicho uliofanyika katika ukumbi wa St Gasper jijini Dodoma.

Kwa mujibu wa Rais wa CWT, Leah Ulaya, uamuzi wa baraza kuu umefikiwa baada ya Maganga kushindwa kupata kibali cha kufanya kazi CWT kutoka kwa mwajiri wake.

Amesema baraza hilo baada ya kujadili hoja hizo limeona kwa mujibu wa utaratibu uliowekwa, Maganga hawezi kuendelea kuitumikia nafasi ya katibu mkuu CWT.

Ulaya alisema wakati baraza hilo likiendelea kujadili suala hilo, ndipo aliposimama katibu mkuu Maganga na kudai licha ya kikao hicho kufunguliwa na rais, bado hana imani naye kutokana na sababu mbalimbali za kiutendaji.

Ulaya ameeleza kuwa hali hiyo ilizua sintofahamu kiasi cha kulazimu vyombo vya usalama kuingilia kati kumkamata katibu huyo na wafuasi wake waliokuwa wameibua vurugu.

Mbali na katibu mkuu, wajumbe wengine waliokamatwa ni
Khamisi Mmtundua, Mwenyekiti Mkoa wa Singida, Alfoncy Mbasa; katibu mkoa wa Morogoro, Paulo Costan; Mwenyekiti Mkoa wa Kagera, Hamisi Chinahova na Katibu Mkoa wa Mwanza, Alen Shuli.

Wengine ni Katibu mkoa wa Shinyanga, Aristides Ishengoma; Mweka hazina Mkoa wa Mwanza, Mahanya Kyola.

Post a Comment

0 Comments