Ticker

10/recent/ticker-posts

Muone nyota huyu mpya wa Yanga, Ally Kamwe asema Tumepata Mtu sahihi

 Baada ya kukamilisha usajili wa Mshambuliaji wa kimataifa wa Ivory Coast, Joseph Guede na kumtambulisha rasmi usiku wa kuamkia jana Jumanne (Januari 16), uongozi wa Young Africans umechimba mkwara mzito kuwa sasa wapinzani wajiandae kisaikolojia kwani, mchezaji huyo atatikisa Bongo kwa rekodi ya mabao.


Usiku wa kuamkia jana Jumanne Young Africans walimtangaza Guede ambaye alikuwa usajili wa tatu kutambulishwa ndani ya klabu hiyo mara baada ya Shekhan lbrahim na Augustine Okrah.

Nyota huyo ambaye ana uzoefu mkubwa wa soka la kimataifa akiwahi kupita kwenye baadhi ya timu kubwa za Afrika na baadhi ya timu kutoka barani Ulaya, ndiye anatajwa kuwa mrithi sahihi wa Mkongomani, Fiston Mayele.

Akizungumzia usajili wa Mshambuliaji huyo, Ofisa habari wa Young Africans, Ally Kamwe amesema baada ya subira ya muda mrefu ya Wananchi, sasa wamepata mtu sahihi wa kurithi nafasi ya Mayele huku akiwaonya wapinzani wao.

“Lilikuwa ni ombi la muda mrefu la mashabiki wetu kupata Mshambuliaji mwenye uwezo mkubwa kama ambavyo ilikuwa kwa, Fiston Mayele na uongozi kupitia ripoti ya kocha mkuu Miguel Gamondi umefikia uamuzi wa kumleta Joseph Guede.

“Kupitia usajili huu nawaonya wapinzani wetu kuwa waandae safu zao za ulinzi vizuri la sivyo hii kasi ya kuwapiga watu magoli mengi itaongezeka maradufu.”

Post a Comment

0 Comments