Ticker

10/recent/ticker-posts

Mchezaji Jean Baleke Atupia la 7, Awafikia Aziz Ki na Max

 Mshambuliaji wa Simba SC, Jean Baleke amefunga goli lake la 7 katika msimu huu wa Ligi Kuu ya NBC katika mechi dhidi ya Namungo FC na kuwafikia nyota wa Yanga SC, Aziz KI na Max Nzengeli ambao wana idadi hiyo ya magoli.

Hiyo ni baada ya Ligi Kuu ya NBC msimu wa 2023-24 kufikia raundi ya tisa lakini Simba akiwa na kiporo kimoja mkononi, mechi dhidi ya Mashujaa FC.

Simba mpaka sasa, wapo kwenye nafasi ya tatu kwenye msimamo wakiwa na alama zao 19 nyuma ya Azam FC wenye alama 19 wakiwa juu kwa tofauti ya magoli ya kufunga na kufungwa huku nafasi ya kwanza ikishikiliwa na Yanga SC wenye alama 24

Post a Comment

0 Comments