Ticker

10/recent/ticker-posts

Raia wawili wa Marekani Waliotekwa Wakutwa Wamekufa Mexico

 Raia wawili wa Marekani kati ya wanne waliotekwa Ijumaa iliyopita nchini Mexico, wamepatikana wakiwa wamekufa. Marafiki hao waliokuwa wakienda Mexico kwa ajili ya upasuaji wa kupunguza tumbo, walitokea katika jimbo la North Carolina wakapita Texas na baadae kuingia Mexico.Walipofika mji wa Matamoros walitekwa na watu wenye silaha. Kupatikana kwao kumekuja baada ya ushirikiano mkubwa kati ya maafisa wa Marekani na Mexico. Matamoros ni moja ya miji hatari sana nchini Mexico inayofahamika kwa uhalifu unaoongozwa na makundi ya wadau wa dawa za kulevya. Makundi hayo yana nguvu kubwa wakati mwingi kuizidi mamlaka. Ni moja kati ya miji 6 ya Mexico ambayo raia wa Marekani wamekuwa wakishauriwa kutokwenda kwa sababu za kiusalama.

Post a Comment

0 Comments