Ticker

10/recent/ticker-posts

Mbowe amemtangaza Rais Samia kuwa ndiye mgeni rasmi kwenye tukio hili kubwa la Chadema

 

Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa Mgeni rasmi katika Maadhimisho ya Siku ya Wanawake wa CHADEMA (BAWACHA) Kitaifa yatakayofanyika Mkoani Kilimanjaro March 08,2023.

Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe ametangaza hilo leo wakati wa Mkutano wake na Waandishi wa Habari Jijini Arusha leo.

Mbowe amenukuliwa akisema “Rais Dkt. Samia atakuwa Mgeni rasmi kwenye tukio la kina Mama siku ya Wanawake duniani, tumemualika na amekubali mimi nitakuwepo Moshi kumpokea”- Mbowe

Post a Comment

0 Comments