Ticker

10/recent/ticker-posts

Baba Majaliwa Afunguka na kusema "Hela Alizopata Mwanangu ni Bora Mimi na Mama yake Tungeshirikiana Tumtunzie"

 

Nilivyosema Majaliwa ni mwanangu watu walibisha, kinachoingia katika familia ni cha familia - Baba Majaliwa
"Mimi na Mama Majaliwa tumetengana kwenye mambo ya ndoa lakini tupo pamoja sana hayupo mbali na mimi na mimi sipo mbali naye kwenye masuala ya familia tunashirikiana kupanga mambo ya familia" - Jackson Majaliwa ameimbia Clouds FM
Kuhusu zawadi alizopewa kijana wao huyo kwa kuvunja mlango kuokoa waliotumbukia na ndege ziwa Victoria, amesema

"Anachokipata tungeshirikiana mimi na familia kama ni kuiweka pesa yake aikute wakati anaendela kukua , tutaangalia kipi tumuhifadhie kwa sababu bado ana wadogo zake na sisi wazazi wake maisha yetu ni ya kawaida sana
"kikubwa tungemuwekea yeye kidogo tungeona namna ya kuwasaidia wadogo zake maana kinachoingia katika familia ni kwa ajili ya familia" - Baba mzazi wa Majaliwa akiongea na Clouds FM


Post a Comment

0 Comments