Ticker

10/recent/ticker-posts

TANZANIA YAITAKA JUMUIYA YA KIMATAIFA KUWEKA MAZINGIRA SAWA YA BIASAHARA



Tanzania imeitaka Jumuiya ya Kimataifa kuhakikisha uwepo wa uwanda na vigezo sawa vya kibiashara ili kuliwezesha bara la Afrika kushiriki kikamilifu katika uchumi jumuishi sambamba na kuwa na mpango kabambe wa kumaliza migogoro katika Nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) baada ya njia ya kijeshi inayotumiwa na Jumuiya ya Kimataifa kutozaa matunda.

Akihutubia kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika Mkutano wa 74 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa unaofanyika New York,Marekani,Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi ameiambia Jumuiya ya Kimataifa kuwa baada ya mbinu za kijeshi kutumika kutafuta suluhu katika Nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kushindikana wakati umefika wa kutafuta majawabu mapana zaidi kuhusu hali ya usalama nchini humo.

Mbali na kutaka Jumuiya ya Kimataifa kuwa na mpango kabambe juu ya utatuzi wa migogoro katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo,pia Tanzania imeitaka Jumuiya hiyo kuondoa vikwazo dhidi ya Zimbambwe huku ikisisitizwa kuwa wanaoteseka katika suala hilo ni wanawake,watoto na wazee wakati ambapo jambo lililosababisha Zimbabwe kuwekewa vikwazo halipo tena.

Pia Tanzania imetoa msimamo wake wa kuendelea kuiunga mkono Umoja wa Mataifa kwa madai ya uwepo wa vitendo vya baadhi ya Mataifa Makubwa dunani kuupuuza Umoja wa Mataifa na kwamba inabariki mageuzi ya kimfumo na utendaji yanayofanyika katika umoja huo na kutoa wito kwa Mataifa ulimwenguni kuheshimiana.

Pro. Kabudi ametoa shime kwa Nchi za Bara la Afrika kuanza kutumia rasilimali na malighafi zake ili kujiletea maendeleo kwa kuwa Bara hilo ni tajiri licha ya kulazimishwa kuwa masikini na kwamba wakati sasa umefika kwa Afrika kujitegemea kwa kutengeneza bidhaa zake na kuondoa tatizo la ajira kwa vijana bara hilo badala ya kugeuzwa soko la Mataifa yaliyoendelea na sehemu ya kuchukulia malighafi ya kuendleza viwanda katika mabara mengine.

Pia ameitaka Jumuiya ya Kimataifa kuhakikisha uwepo wa uwanda na vigezo sawa vya kibiashara jambo litakaloliwezesha bara la Afrika kushiriki kikamilifu katika uchumi jumuishi na kuongeza uwezo wa kibiashara.

Mara baada ya kumaliza kuhutubia katika Mkutano mkuu wa 74 wa Baraza la Umoja wa Mataifa mabalozi na viongozi mbalimbali kutoka bara la Afrika,Marekani,Ulaya na Asia walijipanga mstari na kumpongeza Prof. Palamagamba John Kabudi kwa hotuba yake thabiti na ya kusisimua ambayo imeweka misimamo mbalimbali kwa manufaa ya mataifa yote. 
Posted: 28 Sep 2019 09:00 AM PDT
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi akihutubia katika Mkutano wa 74 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Jijini New York, Marekani.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi akihutubia katika Mkutano wa 74 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Jijini New York, Marekani.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi akiwa katika ukumbi wa Umoja wa Mataifa muda muchache kabla ya hutubia katika Mkutano wa 74 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Jijini New York, Marekani. Kulia ni Waziri wa Afya wa Zanzibar Mhe. Hamad Rashid Mohamed akifuati na Waziri wa nchi,Ofisi ya Makamu wa pili wa Rais zanzibar, Mhe. Mohammed Aboud Mohammed na nyuma ya Prof. Kabudi ni Balozi Ali Abeid Amani Karume. 

Ukumbi wa mikutano wa Umoja wa Mataifa kunaofanyika Mkutano wa 74 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa uliopo New York,Marekani.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (mwenye tai nyekundu katikati) akiwa katika  picha ya pamoja na baadhi ya viongozi muda mfupi baada ya kumaliza kuhutubia katika Mkutano Mkuu wa 74 wa Baraza kuu la Umoja wa Mataifa,New York Marekani.

Baadhi ya viongozi na watumishi wa Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa New York,Marekani wakiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) muda mfupi baada ya kumaliza kuhutubia katika mkutano mkuu wa 74 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, New York,Marekani.


from CCM Blog https://ift.tt/2mGWeBe
via

Post a Comment

0 Comments