Ticker

10/recent/ticker-posts

Serikali Kutenga Bajeti Kwa Ajili Ya Uzalishaji Wa Pamba Mbegu Vipara

Serikali Kutenga Bajeti Kwa Ajili Ya Uzalishaji Wa Pamba Mbegu Vipara
Serikali imeeleza kuwa imejipanga kuimarisha zao la Pamba ili kuongeza uzalishaji nchini kwani kufanya hivyo wakulima watanufaika katika uzalishaji wenye tija na kuimarisha biashara.

Ili kuongeza uzalishaji wa Pamba dhamira ya serikali ni kuanzisha Pamba mbegu vipara ili kuondokana na utumiaji wa pamba manyoya ambayo imezoeleka lakini tija yake ni ndogo katika uzalishaji kuliko Pamba Manyonya.

Naibu Waziri wa Kilimo ameyasema hayo  tarehe 28 Februari 2019 wakati akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Muhunze kilichopo katika Wilaya ya Kishapu wakati wa ziara ya Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan Mkoani Shinyanga.

Alisema kuwa elimu itatolewa kuhusu matumizi ya Pamba mbegu vipara ili kuwajengea uelewa wananchi na serikali kufikia hatua ya kufungamanisha kilimo cha Pamba na uchumi wa viwanda.

Mhe Bashungwa aliongeza kuwa serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mhe Rais Dkt JKohn Pombe Magufuli imejipanga kuhakikisha kuwa kilimo kinawakomboa wananchi ili kuimarisha uchumi wa mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla wake.

“Sisi kama Wizara tutakuwa na jukumu la kushawishi wawezaji ili kuwekeza kwenye viwanda vya Pamba nyuzi pamoja na viwanda vya nguo na kufanya hivyo tutakuwa tumetekeleza vyema maelekezo yaliyoainishwa kwenye ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi yam waka 2015-2020” Alikaririwa

Aidha, alisema kuwa Wizara ya Kilimo imejipanga vyema katika kutafuta masoko ya mazao ya wakulima ambapo kwa upande wa zao la mahindi tayari soko limepatikana kupitia Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) imesaini mkataba wa mauziano ya mahindi ya Tani 36,000 na Mpango wa Chakula Duniani (WFP).

Katika hatua nyingine alisema kuwa wakulima wa Wilaya ya Kishapu ni miongoni mwa wakulima wa zao la Mtama hivyo kupitia Mpango wa Chakula Duniani (WFP) serikali ya Tanzania inaendelea kujiridhisha uhitaji wa mtama nchini Sudani Kusini ili kuwaunganuisha wakulima na soko hilo.

Katika hatua nyingine Naibu Waziri huyo ameiagiza Bodi ya Pamba kuhakikisha viuadudu (Viuatifu) vinapatika haraka katika Wilaya ya kishapu ili kuondoa haraka changamoto inayowakumba wakulima kwa kukosekana viuatilifu kwa wakati.



from UDAKU SPECIAL BLOG https://ift.tt/2T9Pkn4
via

Post a Comment

0 Comments