Ticker

10/recent/ticker-posts

Haya ndio yanasadikika kuwa ni mapenzi ya kweli

Nguli wa fasihi Tanzania alishawahi kuongelea mapenzi bora katika kitabu chake kiitwacho Mapenzi bora.

Nguli huyu SHABAN ROBERT alihimiza sana swala la mapenzi bora hii ni kwa sababu mapenzi bora huleta afya, mapenzi bora huleta amani ushilikiano na upendo,mapenzi bora hujenga familia bora mno, mapenzi bora pia huwa kinga ya magojwa, na mapenzi bora ni dawa na tiba.
Yapi ni mapenzi bora: 

1 Kupeana ushauri mwema wa mahusiano yenu, 
2 Kuulizana kipi mwenza wako anapenda na kipi hapendi, 
3 Kuliwazana pale kunapokuwa na huzuni (kuwa mfariji mwema), 
4 Kuepuka ugomvi usokuwa wa lazima, 
5 Kushilikiana katika kuleta maendeleo mema ya kifamilia na kijamii, 
6 Kuonesha upendo kwa dugu,jamaa,marafiki na watu wote wa karibu yenu, 
7 Ucha Mungu