Kikwete ametoa sifa hizo kwa Wachaga, huku akiyahusisha baadhi ya makundi ya watu nchini, ambayo hata kulima kwa ajili ya mlo wao wanalazimika kusukumwa.
Kikwete ametoa kauli hiyo jana Jumatatu, Desemba 23, 2024 alipowaongoza maelfu ya wanariadha katika mbio za Rombo Marathon zilizofanyika katika Hifadhi ya Msitu wa Rongai wilayani Rombo, Kilimanjaro.
"Kuna maeneo hapa nchini watu hata kujilimia chakula chao inabidi usukumane nao, lakini hakuna Mchaga utakayemsukuma kwa kujiletea maendeleo, na hiyo ndio siri, uzuri Wachaga hawasahau kwao kila mwaka wanakwenda kuhesabiwa," amesema.
Kwa mujibu wa Kikwete, mtindo wa kwenda nyumbani kila mwisho wa mwaka unajenga ushawishi kwa wengine kuonyesha hatua za maendeleo walizopiga.
"Niwapongeze wananchi wa Rombo kwa moyo wenu wa kujituma na kujiletea maendeleo, mimi nimefanya kazi wilayani, mkoani, wizarani na katika ngazi ya juu kabisa ya uongozi wa nchi yetu, Watanzania wote wangekuwa na ari ya wachaga nchi yetu ingepiga hatua kubwa, endeleeni na moyo huo," amesema.
(Imeandikwa na Janeth Joseph)
#mwananchiupdates
#tunaliwezeshataifa