Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini (TARURA) Mhandisi Victor Seff amesema TARURA kupitia mradi wa RISE unaendelea na zoezi la ukaguzi wa Miradi yote ya Bottleneck katika mikoa yote ili kuhakikisha kazi hizo zinakamilika kwa wakati.
Wataalamu kutoka wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini (TARURA) wanaokagua miradi hiyo kwa Mikoa ya Mara na Simiyu wakiongozwa na Mhandisi Ephrahim Kalunde wamefanya ukaguzi wa maendeleo ya kazi za ujenzi wa mradi wa uondoaji vikwazo vya miundombinu (Bottleneck Intrventions) inayotekelezwa chini ya Mradi wa RISE Unaofadhiliwa na Benki ya Dunia kwa mkopo wa masharti nafuu
Akiongea na mwandishi wa habari hii mratibu wa zoezi hilo baada ya kumaliza ukaguzi katika wilaya za Bunda,Butiama,Musoma,Tarime,Rorya na Serengeti Mkoani Mara Mhandisi Kalunde amesema lengo la kukagua miradi hii ni kutekeleza agzo la MtendajiMkuu wa TARURA Mhandisi Victor Seff la kuhakikisha kila kazi inasimamiwa na kwisha kwa wakati kama mikataba ilivyoainisha.
Naye Mataalamu wa Mazingira naMasuala ya Jamii toka TARURA Bi Domina Mgoma amesema maelekezo ya Mtendaji Mkuu pamoja na Benki ya Dunia ni kuhakikisha taratibu za kisheria kwenye masauala ya jamii na mazingira zinafuatwa na kuona utekelezaji wake ili jamii iwe salama sasa na baada ya kumalizaka kwa kazi.
Akiongea katika ziara hiyo Mtaalamu wa Masuala ya Ununuzi na Ugavi Bw.Kennedy Elimeleck amesema kwenye upande wa ununuzi Taratibu zote zipo sawa na sasa kikubwa ni kuhakikisha mikataba yote inakamilika kwa wakati ili kuepuka ucheleweshaji wa barabara,vivuko na madaraja mbalimbali yanayotekelezwa kukabidhiwa kwa wananchi jambo ambalo amesema ni kiu kubwa ya Mtendaji Mkuu Mhansisi Victor Seff kutaka kuona kazi zote za Bottleneck zinakamilika kwa wakati na kwa thamani ya fedha (Value for Money).
Naye mmoja wa wataalamu hao ambaye ni mtaalamu wa fedha CPA Obed Nzogela amesema wao wanajitahidi kuhakikisha wakandarasi wanalipwa kwa wakati ili kuepuka kazi kusimama na kupelekea miradi hiyo kuchelewa.
Ziara hiyo ya ukaguzi wa Miradi inaendelea katika mikoa ya Mara na Simiyu ambapo Mameneja wa Mikoa na Wilaya wamefurahishwa na zoezi hilo lenye lengo la kusimamia utekelezaji wa kazi za ujenzi wa miradi hiyo inayoonekana kuwa na tija kubwa kwa wananchi.
Aidha katika ziara hiyo wataalamu hao ambao wameambatana na Mtaalamu Mshauri wa Miradi hiyi yaani 'Project Management Consultant' (PMC) Mhandisi Kiiza wamesema kazi zinaenda vizuri na siku chache zijazo kazi hizo zinatarajia kukamilika.