Eng.VICTOR SEFF wa TARURA ashinda Tuzo ya Mtendaji Mkuu Bora wa Mwaka 2023/2024 Jijini Dar es Salaam

Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) Mhandisi Victor H. Seff ameshinda  tuzo ya utendaji bora na kuwa miongoni mwa Watendaji  Wakuu 100 na kuwa kinara katika tuzo hizo kwa mwaka 2024, katika  kipengele cha Mtendaji Mkuu wa mwaka(CEO/MD of the year).

Tuzo hiyo imetolewa usiku wa tarehe 24 Novemba,2024 katika ukumbi wa 'The Super Dome' uliopo Masaki Jijini  Dar es Salaam.

Mgeni rasmi katika hafla hiyo kwa Upande wa Serikali alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Kazi, Uchumi na Uwekezaji Zanzibar Mhe. Sharrif Ali Sharrif.

Akizungumza mara baada ya kupokea tuzo hiyo Mhandisi Seff aliwashukuru waandaaji wa tuzo hizo, Kampuni ya Eastern Star Consulting Group Ltd, Ofisi ya Rais -Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) pia watumishi wote wa TARURA kwa ushirikiano wao katika utendaji wa kazi ambapo imemuwezesha kupata tuzo hiyo na kuwa wa kwanza kati ya Watendaji wakuu zaidi ya 100 waliopendekezwa.

Amepata tuzo kutokana na Vigezo vilivyowekwa na waandaaji wa Tuzo hizo ambapo vilikuwa vinahitaji:-

  • Mtendaji Mkuu ambaye ametoa mchango mkubwa zaidi kwenye sekta yake au sekta fulani (TARURA ikiwa ni kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa Barabara za Mijini na Vijijini).
  • Mtendaji Mkuu ambaye ametoa Mchango Mkubwa kwa Taifa kupitia Taaluma au eneo analosimamia
  • Mtendaji Mkuu wa Taasisi yenye Tija Kwa nchi na Wananchi kuanzia ngazi za Chini hadi Juu.
  • Mtendaji Mkuu wa Taasisi inayofanya kazi na jamii pamoja na kugusa amoja kwa moja maendeleo ya ngazi za chini.
  • Mtendaji Mkuu Mwenye Rekodi isiyopingika katika kusimamia miradi yenye matokeo makubwa kwa wananchi au serikali.

Tuzo  hiyo inayojulikana kama  ‘Top 100 Executive List Awards’ ni mara ya tano kufanyika Nchini na imeandaliwa na Kampuni ya Eastern Star Consulting Group Limited inayotoa tuzo kama hizo kwa nchi zaidi ya tano ikiwepo Kenya,Tanzania,Uganda,Falme za Kiarabu(U.A.E),Afrika Kusini nk.

Akiongea baada ya Mhandisi Seff kukabidhiwa Tuzo hiyo Mkurugenzi wa Kampuni ya Eastern Star Consulting Group Bw.Deogratius Kilawe amesema wanazishukuru Taasisi zote pamoja na Makampuni zaidi ya 3000 zilizopendekeza majina katika vipengele mbalimbali ambapo katika kipengele cha Mtendaji Mkuu Bora Mtendaji Mkuu wa TARURA Mhandisi Victor Seff ameibuka Mshindi.

Aidha Kilawe amempongeza Mhandisi Seff kwa kuwa tofauti na ilivyozoeleka kwa Taasisi za Umma ambazo huwa zinashiriki tuzo hizo yeye Mhandidi Seff alipata kura nyingi za Kishindo zilizopigwa na Wafanyakazi wa TARURA Nchi Nzima pamoja na Tasisi Nyingine,Wananchi wa Kawaida na Viongozi mbalimbali wakiwepo Wabunge,Mawaziri Pamoja na Madiwani bila kuwasahau wananchi wa Kawaida ambapo Kilawe amesema hii ni ishara tosha ya kuonyesha ni kwa jinsi gani Mhandisi Seff ni mtu mwenye mchango mkubwa kwa Taasisi anayoiongoza ya TARURA,Viongozi wengine na wananchi kwa ujumla.

Akiongea baada ya Ushindi wa Tuzo hiyo Muhimu Mhandisi Seff alisema "Mabibi na Mabwana,napenda nitoe Shukrani zangu za Dhati kwanza Kwa Mwenyezi Mungu,Mke wangu na Famila yangu,Wafanyakazi Wote wa TARURA kwa kujitoa kwao kunitia moyo,kunisaidia na kunipigia kura katika Kinyang'anyirio hichi,Nawahukuru sana.

Katika Tuzo hizo Mtendaji Mkuu huyo aliambatana na Timu nzima ya TARURA Makao Makuu ikiongozwa na Mkurugenzi wa Huduma Saidizi Bi.Azimina Mbilinyi,Mkurugenzi wa Barabara Mhandisi Venant Komba,Mkurugenzi wa Mipango ya Miundombinu Mhandisi Edward Amboka,Mkurugenzi wa Ununuzi Bi.Ziada Msangi,Mhasibu Mkuu TARURA CPA Jacob Nyaulingo,Mkuu wa Kitengo cha Miradi ya Benki ya Dunia Mhandisi Humprey Kanyeye,Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano kwa Umma Bi Catherine Sungura,Mwenyekiti wa Mameneja wa TARURA wa Mikoa ambaye Pia ni Meneja wa Mkoa wa KIlimanjaro Mhandisi Nicolaus Francis,Meneja wa TARURA Mkoa wa Pwani Mhandisi Leopold Lunji pamoja na Meneja wa TARURA Mkoa wa Dar es Salaam Mhandisi Geofrey Mkinga.

Previous Post Next Post

نموذج الاتصال