BREAKING:Haya hapa majina ya Vituo vya Treni ya SGR,yapitishwa na Mhe.Rais Samia Rasmi

 

Rais Samia Suluhu Hassan ameridhia stesheni ya Reli ya Kisasa ya SGR ya mkoani Dodoma kuitwa jina lake na sasa itajulikana kama Samia Station huku stesheni ya Dar es Salaam ikipewa jina la mtangulizi wake, Hayati Dkt. John Pombe Magufuli.

Akitangaza majina ya stesheni zote za reli ya SGR, Rais Samia amsema, Stesheni ya Morogoro itaitwa jina la Rais wa awamu ya Nne, Jakaya Kikwete huku ile ya Tabora ikipewa jina la Rais wa awamu ya Pili, Mzee Ali Hassan Mwinyi

Stesheni ya Shinyanga imepewa jina la Rais wa Kwanza wa Zanzibar, hayati Abeid Aman Karume, Stesheni ya Mwanza itaitwa Julius Nyerere na Kigoma mwisho wa Reli, itaitwa Benjamin Mkapa.


Previous Post Next Post

نموذج الاتصال