Ticker

10/recent/ticker-posts

Wananchi Lindi Kufanyiwa jambo Hili Kubwa na muhimu na TPDC

Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) kwa kushirikiana na Kampuni za Kimataifa za Nishati, Shell na Equinor imetoa elimu ya ushiriki wa wananchi katika mradi wa ujenzi wa Shule  ya Msingi  Likong'o iliyopo Kata ya Mbanja, Manispaa ya Lindi.

Shule hiyo, ambayo ujenzi wake utaanza hivi karibuni inatafsiri kwa vitendo jitihada za TPDC kwa kushirikiana na Wawekezaji wa mradi wa kusindika gesi asilia  (LNG), kuimarisha huduma za kijamii na kuchangia maendeleo ya wananchi wanaozungukwa na mradi wa LNG ambao unatarajia kutekelezwa Mkoani Lindi.