Ticker

10/recent/ticker-posts

Mo Dewji Athibitisha Kurudi Kuwa Mwenyekiti wa Bodi Simba, Amrudisha Try Again

 

Mwekezaji wa Simba SC Mohammed Dewji (MO) ametoa taarifa rasmi kuhusiana na kinachoendelea Simba SC baada ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi Salim Abdallah Muhene Try Again kutangaza kujiuzulu pamoja na Wajumbe wa upande wa Muwekezaji.MO Dewji amethibitisha kuwa anarejea tena kuwa Mwenyekiti wa Bodi wakati Try Again anarudi katika Bodi kama Mjumbe wa upande wa Mwekezaji na tayari Try Again ameridhia pendekezo hilo.

“Nilimchagua Ndugu Salim kuwa Mwenyekiti wa Bodi kwakuwa nimeshafanya kazi nae muda mrefu, namjua ni Mtu muaminifu na mtulivu namshukuru sana na Wajumbe wote wa Bodi kwa kazi kubwa waliyoifanya mpaka sasa”“Nimeshauriana na Viongozi mbalimbali pamoja na Bodi ya ushauri chini ya Jaji Mihayo na kukubali ombi la kuwa Mwenyekiti wa Bodi kwenye hiki kipindi kigumu mpaka Simba itakaporejea kwenye hali yake, nimemuomba Salim kubaki kwenye Bodi kwa niaba ya Muwekezaji na amekubali na hivi punde nitateua wengine kujaza nafasi ili Bodi iwe kamili” ——— Dewji