Ticker

10/recent/ticker-posts

Hii ndiyo Masama English Medium School,Moja ya Shule Bora kabisa Nchini Tanzania Kwa sasa,Mpeleke Mwanao


 Masama English Medium Pre & Primary School ni moja ya Shule zinazofanya Vizuri kwa Matokeo  ya elimu ya Shule ya Msingi kwa Sasa Nchini Tanzania ambapo imeshika nafasi ya Kwanza Kiwilaya ndani ya wilaya ya Hai kwa miaka mitano mfululizo kwa matokeo ya Darasa la Saba ambapo ina nafasi za kutwa na bweni kwa wanafunzi wanaotoka maeneo mbalimbali nchini Tanzania bila kuabagua Dini wala kabila.

Masama English Medium Pre & Primary School ipo katika Kijiji Cha Mbweera Kata ya Masama Mashariki Wilayani Hai Mkoani Kilimanjaro ambapo iliasisiwa na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Usharika wa Masama Kati.

Akiongea kwa niaba ya Washarika wa Usharika wa Masama Kati ambao ndipo shule Hiyo ilipo Mchungaji kiongozi wa Usharika wa Masama Kati Mchungaji Praygod Usiri amesema wanawakaribisha wazazi na walezi wa watoto wote kokote nchini kuwaleta watoto wao katika shule hiyo ili wapate elimu bora na malezi bora kwani shule hii kwa sasa ni moja ya shule zinazofanya vizuri kiwilaya,kimkoa na hata kitaifa ambapo ada zao ni nafuu sana.

Kwa maulizo zaidi unaweza kuongea na Viongozi wa Shule hiyo kwa namba 
0678606593 au 0754952558