Ticker

10/recent/ticker-posts

SHUHUDIA CHONGOLO ALIVYOLALA KWA MWENYEKITI WA SHINA NAMBA 35 (BALOZI WA NYUMBA 10) HUKO SIMANJIRO

 

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo akiendelea na ziara yake mkoa wa Manyara wilayani Simanjiro amelala  nyumbani kwa mwenyekiti wa shina namba 35,  Tawi la Njiro Kata ya Orkesumet kwa Bwana Abdul Mwinyihamisi, ikiwa ni sehemu ya Chama kushuka kwa Wanachama. 

Chongolo amewashukuru sana na kuwapongeza  wenyeviti wa mashina nchi nzima kwa kuwa na moyo wa kujitolewa wa kufanya kazi wakati wote wa ujenzi wa Chama, katika imani ya Chama ya utu, usawa na udugu, ambapo amewaomba kuendelea hivyo kwani moyo huo ndio msingi wa uimara wa chama chetu.

Chongolo yupo mkoani Manyara kwa ziara ya kukagua utekelezaji wa  Ilani, kuimarisha uhai wa chama pamoja na kusikiliza na kutatua kero za wananchi, ambapo ameambatana na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Sofia Mjema pamoja na Katibu wa NEC, Oganaizesheni Issa Haji Gavu.Chapisha Maoni

0 Maoni