Faida za biashara ndogo ndogo Tanzania pamoja na manufaa na umuhimu wa kuanzisha biashara yako ndogo na yenye mtaji kidogo.
1. Wewe Ndio Unakuwa Mmiliki wa Biashara
Unapoanzisha biashara yako ndogo, wewe pekee au wale ulioanzisha nao ndiyo mnakuwa wamiliki wa biashara hiyo na hivyo mnakuwa na udhibiti mkubwa wa biashara.
Umiliki na udhibiti wa biashara unapobaki kwa watu wachache, unafanya biashara iweze kuendeshwa vizuri na kuweka vizuri vipaumbele vya biashara hiyo.
Unapochagua kubaki na biashara ndogo, unabaki na umiliki na udhibiti wa biashara hiyo na kuweza kufanyia kazi vipaumbele sahihi vya biashara bila ya kushinikizwa na yeyote.
2. Uhuru wa Kufanya Kile Unachokipenda
Biashara inapokuwa ndogo na udhibiti uko kwako unaweza kufanya maamuzi na asiwepo yeyote wa kukusumbua.
Lakini biashara inapokuwa kubwa na ina wamiliki wengi, hawawezi kukubaliana na wewe kuacha faida kwa sababu ya kuangalia mapenzi yako.
3. Mahusiano Mazuri na Wafanyakazi
Kwenye biashara ndogo, ambayo ina wafanyakazi chini ya mia moja, mmiliki wa biashara anakuwa anamjua kila mfanyakazi kwa jina lake na sifa zake.
Wafanyakazi wanakuwa wanajuana kwa majina na sifa zao Hii inaleta ushirikiano mkubwa sana, watu wanashirikiana kama timu moja, kwa sababu wanajuana vizuri.
4. Kujenga Mahusiano Mazuri na Jamii
Mahusiano mazuri baina ya jamii na biashara ni nguzo muhimu sana kwenye uimara wa biashara yoyote ile na Biashara nyingi kubwa huwa zinayajenga mahusiano haya kupitia utoaji wa misaada na huduma mbalimbali za kijamii.
5. Mahusiano Mazuri na Wateja
Biashara inapokuwa ndogo, mmiliki wa biashara anakutana na wateja wa biashara hiyo kila siku na hivyo kusikia moja kwa moja kutoka kwao, kupata maoni yao, kujua changamoto zao na hata kuona fursa zaidi za kuwahudumia wateja hao.
Unapokuwa na biashara ndogo, ambapo wewe mmiliki bado unapata nafasi ya kukutana na wateja moja kwa moja, mahusiano na wateja yanakuwa bora na wanaitegemea zaidi biashara.
6. Uhuru wa kuwa na Uongozi Unaoutaka
Unapoendesha biashara ndogo, unachagua ni aina gani ya uongozi unaotaka kuwa nao kwenye biashara yako na Hulazimiki kufuata uongozi fulani kama makampuni makubwa ambayo yana wawekezaji.
7. Uwezo wa Kutumia Fursa Vizuri
Ukiwa na biashara ndogo, maamuzi yanafanywa na watu wachache, hivyo inapojitokeza fursa yenye manufaa, mnaweza kufikia maamuzi haraka na kunufaika na fursa hiyo.
0 Maoni