Ticker

10/recent/ticker-posts

TARURA WAANZA KUTUMIA TEKNOLOJIA MBADALA UJENZI WA BARABARA,WAANZA NA MOJA YA BARABARA MUHIMU ZA DODOMA

Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini TARURA tayari imeanza kutekeleza ushauri wa wadau mbalimbali ikiwepo viongozi wa serikali ikiwataka waanze kutumia teknolojia mbadala ambayo ni ya gahrama nafuu na inayopunguza uchafuzi wa mazingitra huku kazi ya ujenzi ikikamilika kwa haraka na kwa ubora pia.

Akizungumza na mwandishi wa makala hii Mtendaji Mkuu wa TARURA Mhandisi Victor Seff amesema TARURA kama mdau na mmoja wa Taasisi yenye dhamana ua ujenzi wa barabara za vijijini na mijini tayari wamepokea mawazo na ushauri wa viongozi mbalimbali juu ya kitumia teknolojia mbadala katika ujenzi wa barabara  inzaojenga Vijijini na Mijini kwani ni  Teknolojia iliyothibitishwa kwa zaidi ya miaka kumi na tano ya majaribio ya maabara na nyanjani.

Mhandisi Seff amesema Sisi kama Taasisi iliyopewa dhamana ya ujenzi wa barabara za Mijini na Vijijini tumeangalia mambo mengi Muhimu kabla ya kuanza kutumia teknolojia hii ambapo kati ya hayo hii teknolojia inasaidia mambo yafuatayo:-

• Hupunguza kiwango cha kaboni katika mchakato wa ujenzi hadi 75%.hivyo ni salama zaidi kwa mafundi,watu miaji wa barabara na nazubgira pia.

• Hupunguza gharama za ujenzi wa barabara hadi 50%. hivyo unaweza kutumia fedha kidogo kujenga barabara nyingi.

• Hupunguza gharama za matengenezo ya barabara hadi 60%. kwa sababu zinadumu muda mrefu.

• Imeundwa kwa ajili ya barabara za umma, za kibinafsi, za madini, za kilimo.

• Fomula isiyo na sumu, rafiki wa mazingira kabisa.

• Hakuna vifaa maalum vinavyohitajika kwa taratibu za ujenzi.

Ikumbukwe Tarura sasa kwa kulithibitisha hili imeanza ujenzi wa Barabara iliyoko Ilazo jijini Ddodoma ambapo ujenzi wake unatekelezwa na unatarajia kumalizika kwa kiwango kilichopangwa kwani mkandarasi ameshasaini mkataba na tayari kazi inaendelea alimalizia Mhandisi Seff.

Kwa sasa Teknolojia hiyo ya ujenzi wa barabara inatumika sehemu mbalimbali duniani ikiwepo Visiwani Zanzibar ambapo imeonyesha matokeo bora kwa barabara iilikotumika.

Chapisha Maoni

0 Maoni