Mwandishi wetu leo amefanya mahojiano na mtendaji mkuu wa TARURA na kumweleza kuhusu hatua iliyofikiwa kwa Moja ya Barabara ya Kasulu- Kabanga-Kasumo-Muyama iliyoko wilayani Buhigwe Mkoani Kigoma inayotarajiwa kujengwa kwa kiwango cha Lami ambapo mkandarasi tayari ameshasaini mkataba wa ujenzi huo unaotarajiwa kuchukua kipindi cha mwaka mmoja.
Akizungumza na mwandishi wetu Mtendaji mkuu wa Tarura Mhandisi Victor Seff amesema kuhusu barabara ya Kasulu Kabanga tayari kila kitu kimeshakamilika kuanzia michakato ya kumpata kandarasi hadi mkataba wa ujenzi huo umeshasainiwa hivyo mkandarasi anatarajiwa kuanza kazi hiyo wakati wowote kutoka sasa.
...TARURA tunakuwa na mipango yetu kwa kila mwaka ambapo mwaka huu wa fedha wa 2022/2023 moja ya kazi tuliyopanga kuifanya ni kuhakikisha hii barabara ya Buhigwe inajengwa kwa kiwango cha Lami na yote ina umbali wa kilomita 35 ambapo kwa kuanza tumeanza awamu ya kwanza na kusaini mkataba wa kujenga Kilomita 12.5 kisha baada ya hapo tutaendelea na kipande kitakachobakia.
0 Maoni