Ticker

10/recent/ticker-posts

DKT.MPANGO,MHE.MIZENGO PINDA WAONGOZA MAHAFALI YA 41 YA CHUO KIKUU HURIA,YUPO MHITIMU DKT.HAJI MNASI NA WENGINE

Mkuu wa Chuo Kikuu Huria Cha Tanzania (OUT ) ambaye pia ni waziri mkuu Mstaafu Mhe.Mizengo Kayanza Peter Pinda kushoto akiwa na  Mgeni Rasmi akiwa Makamu wa Rais Mhe.Dkt Philip Isdor Mpango.

 

Baadhi ya wahitimu wa kozi mbalimbali waliohudhuria Mahafali ya 41 ya Chuo kikuu Huria cha Tanzania (OUT)yaliyofanyika  jana kitaifa jijini Mwanza yakiongozwa na Mkuu wa Chuo Hicho ambaye pia ni waziri mkuu Mstaafu Mhe.Mizengo Kayanza Peter Pinda na Mgeni Rasmi akiwa Makamu wa Rais Mhe.Dkt Philip Isdor Mpango ambapo washiriki na   wahitimu mbalimbali walitunukiwa shahada yao ya Uzamivu (PhD)akiwepo aliyewahi kuwa mkurugenzi mtendaji wa wilaya ya Ileje mkoani Songwe bwana Haji Mnasi ambaye amesema ameanza kusoma Shahada Hiyo Mwaka 2018.


Pichani ni Dkt. Haji Mnasi ambaye alikuwa ni mmoja wa wahitimu  wa Shahada ya Uzamivu PhD akifurahi a baada ya kutunukiwa shahada yake hiyo kwenye mahafali yaliyofanyika katika viwanja vya Furahisha jijini mwanza jana tarehe 25/11/2022.Aidha Bwana Manasi ametoa shukrani zake kwa Mwenyezi Mungu,Wazazi wake,Familia yake,Serikali ya Cahama Cha Mapinduzi  na Marafiki zake kwani kila mmoja ametoa mchango mkubwa katika kumaliza shule yake ambapo amesema alianza tangu  mwaka 2018 na moja ya kitu kilichomsukuma kusoma Shahada hii pamoja na umri wake mdogo ni kwa sababu anasema anaona kabisa bado wataalamu wa PhD wanahitajika hasa kuisaidia serikali katika maeneo mbalimbali ikiwepo Taasisi za Elimu ya juu na kwingineko.

Post a Comment

0 Comments