Ticker

10/recent/ticker-posts

PICHA ZA MATUKIO MBALIMBALI YA ZIARA YA KATIBU MKUU CCM NDG.DANIEL CHONGOLO NCHINI BURUNDI

 Pichani ni Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)Ndugu Daniel Chongolo akimvisha medali kapteni wa timu ya K.C.C.A ya Uganda John Revita baada ya kuibuka na ushindi wa magoli 4-0 dhidi ya timu ya Aigle Noir Burundi na kuchukua kombe la Nkurunziza Cup, mechi hii imechezwa kwenye uwanja mpya na wa kisasa wa Nkurunziza Peace Park Complex Makamba nchini Burundi ambapo katika ziara yake hiyo Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Chongolo Ameambatana na Naibu katibu mkuu CCM Zanzibar Juma Mabodi pamoja na Katibu wa Oganaizesheni na Uhusiano wa Kimataifa Kanali Ngemela LubingaKatibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)Ndugu Daniel Chongolo akishuhudia mchezo huo kwenye uwanja mpya na wa kisasa wa Nkurunziza Peace Park Complex Makamba nchini Burundi

Naibu katibu mkuu CCM Zanzibar Juma Mabodi akifurahia jambo katika Tukio Hilo

pamoja na Katibu wa Oganaizesheni na Uhusiano wa Kimataifa Kanali Ngemela Lubinga akijadiliana na kufurahia jambo na mmoja wa viongozi wa CCM katika tukio Hilo
Moja ya Picha katika tukio hilo ikimwonyesha Katibu Mkuu Chongolo akijadili na kufurahia Jambo na mmoja wa Viongozi wa Burundi waliohudhuria wakati wa sherehe za ufunguzi wa uwanja wa michezo wa Nkurunziza Peace Park Complex.
Moja ya Picha katika tukio hilo ikimwonyesha Chifu Mtwale Isambe Rugali Buliho wa himaya ya Heru Juu Buha kasulu Kigoma akionyesha uzalendo kwa majirani zake wakati wa sherehe za ufunguzi wa uwanja wa michezo wa Nkurunziza Peace Park Complex.

Chapisha Maoni

0 Maoni