Ticker

10/recent/ticker-posts

CHONGOLO AFUNGUKA KUHUSU BODABODA KUINGIA KATIKATI YA JIJI LA DAR..SOMA HAPA


Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo  amesema Kwa upande wa zoezi linaloendelea la kuwapanga watu wa bajaji na bodaboda mkoa wa Dar es salaam kuwa watu hao hawawezi kuondolewa katikati ya jiji hilo hivyo wapuuze watu wenye nia ovu ya kuichonganisha wananchi na serikali yao

 Chongolo ameyasema hayo, leo tarehe 22 Aprili, 2022 katika kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM wilaya ya Ilala.

amesema kuwa, hao ni watu muhimu hawawezi kuachwa kwa sababu wanajitafutia riziki halali, ambapo amewasihi watu waache kutoa taarifa za kupotosha umma kuwa wanaondoshwa mjini.

“Kinachofanyika sio kuwazuia bodaboda na majaji wasiingie mjini bali ni kuwaratibu ili kuwawekea vituo rasmi zitavyoweza kutambulisha watu wanahitaji kutumia usafiri huu”, Katibu Mkuu Ndg. Chongolo amesisitiza

Ndg. Chongolo amesisitiza kuwa waendesha bajaji baadhi yao ni watu wenye ulemavu, ambao ni kundi maalum linalopata mikopo inayotolewa na Halmashauri asilimia 10, hivyo lazima waheshimiwe kwa kuwaweka eneo maalum kwa ajili yao ili wasigombanie abiria na watu wengie wasiokuwa na ulemavu.

Katika hatua nyingine, Katibu Mkuu Ndg. Chongolo ametumia mkutano huo kuwakumbusha majukumu wajumbe wa kamati za siasa za ngazi zote wakiwemo viongozi wa Jumuiya ambapo kwa sasa kwa tathimini iliyopo Kamati hizo hazitekelezi majukimu sawasawa hasa kusimamia ajenda za wananchi.



Post a Comment

0 Comments