Ticker

10/recent/ticker-posts

KATIBU MKUU WA CCM MHE. DANIEL CHONGOLO AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA "BALOZI WA MTWARA" JOEL NANAUKA, DODOMA.


Balozi wa Mtwara na Mwandishi wa vitabu nchini  Bw. Joel Nanauka amekutana na kufanya Mazungumzo na katibu mkuu wa CCM Ndugu Daniel Chongolo.
Katika mazungumzo hayo wamejadiliana mambo mbalimbali ikiwemo mchango wa Ndg Nanauka katika program mbalimbali za uimarishaji wa chama  kwa ujumla na program maalumu zinazohusu vijana.Ndg Joel Nanauka , alimpongeza Katibu Mkuu kwa kazi kubwa anayofanya na alimhakikishia kuwa  yuko tayari kuendelea kutoa mchango wake kwa chama kuanzia ngazi ya Taifa hadi chini kabisa Kama ambavyo amekuwa akifanya siku zote. 

Moja kati y avitabu vilivyoandikwa na mwandishi huyu mahiri ambaye ni Balozi wa Mtwara Bwa.Joel Nanauka na vitabu vyake vimeshawanufaisha watanzania wengi.
Ndg Nanauka ambaye ni balozi wa Mtwara, alitumia nafasi hiyo pia kuwasilisha mambo mbalimbali ya kisekta yenye manufaa kwa mkoa wa Mtwara.

Baada ya Mazungumzo, Ndg Nanauka alimkabidhi Katibu Mkuu Zawadi ya baadhi ya Vitabu alivyoandika na kumtakia kila la Kheri katika mkutano Mkuu maalumu wa CCM Taifa unaofanyika tarehe 01.04.2022.

Kabla ya kutoka katika ofisi za makao makuu ya Chama hicho Jijini Dodoma Nanauka alisema
"Binafsi nimefurahi na kufarijika sana kuonana na katibu mkuu wa Chama Chetu cha Mapinduzi Ndugu Chongolo,kwani nimetamani wasaa huu muda mrefu na nimejifunza mengi kutoka kwake pia  tumekuwa na mazungumzo yenye manufaa sana kwetu,na nimemuahidi kutangaza mema yanayofanywa na chama cha mapinduzi kwa wana Mtwara na Watanzania kwa ujumla,Mungu ibariki Tanzania,Mungu mbariki Rais wetu Samia Suluhu Hassan na Kazi Iendelee.
Alimalizia Ndugu Nanauka.

  Picha juu ikimuonyesha Katibu mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Cde Daniel Chongolo leo baada ya kukutana na  Ndg Joel Nanauka na kufanya naye mazungumzo katika ofisi Kuu za CCM jijini Dodoma ambapo Ndugu Nanauka alimpa vitabu ambavyo yeye ndiye mtunzi na mwandishi wa vitabu hivyo kama ishara ya kutambua mchango wa katibu mkuu huyo kwa Chama Cha Mapinduzi..

Post a Comment

0 Comments