Ticker

10/recent/ticker-posts

SOMA HII TAARIFA MUHIMU KUHUSU KAMATI KUU YA CCM KUKUTANA

Kamati Kuu ya Halmashauri  Kuu ya CCM inatarajiwa kukutana Jumanne Juni 22, 2021 chini ya Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan.

Kikao hicho  kimetanguliwa na kikao cha Secretariet ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kilichofanyika chini ya Mwenyekiti wake Katibu Mkuu wa  CCM Ndugu Daniel Chongolo kimefanyika katika ukumbi wa NEC White House Jijini Dodoma 

"Ni kweli Jumanne 22 Juni 2021  Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan ataongoza kikao cha kawaida cha kamati Kuu, maandalizi yote yamekamilika, ni kikao cha kawaida cha Kikatiba" Shaka Hamdu Shaka Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi.Chapisha Maoni

0 Maoni