Ticker

10/recent/ticker-posts

SOMA HII TAARIFA MPYA YA SERIKALI KUHUSU BEI MPYA ZA BANDO 'VIFURUSHI' VYA SIMU

 
Kufuatia malalamiko na mjadala mkubwa mara baada ya kutangazwa kwa bei mpya za vifurushi ambapo matarajio ya wengi ilikuwa ni kushuka kwa gharama hizo leo Aprili 2,2021, Serikali imetangaza kusitisha kutumika kwa gharama hizo hadi hapo itakapotangazwa baadaye.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano kwa Umma wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Semu Mwakyanjala, amesema matumizi ya bei mpya ya vifurushi yamesitishwa kwa muda akieleza kuwa uamuzi huo utahusu vifurushi vya data pekee huku vile vya ujumbe mfupi wa maneno na kupiga zitaendelea kama ilivyotangazwa leo.


Post a Comment

0 Comments