WAZIRI MAMBO YA NDANI ATOA KAULI VIFO VYA WATU 20, ATHIBITISHA JESHI LA POLISI KUMSHIKILIA MCHUNGAJI MWAMPOSA..

  Masama Blog      
.
Na Said Mwishehe, Michuzi Globu ya jamii

SERIKALI kupitia Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi George Simbachawene amesema kutokana na tukio la kufariki dunia kwa watu 20 kwenye kongamano la Mchungaji Mwamposa na kwamba kuna kila sababu ya kuchukua hatua stahiki kwa mchungaji huyo.

Hata hivyo tayari Mchungaji Mwamposa anashikiliwa na Jeshi la Polisi na linafikiria kumuondoa Dar es Salaam na kumpeleka mkoani Kilimanjaro.
Akizingumza leo Waziri Simbachawene amesema kuwa inasikitisha unakuwa na idadi kubwa ya watu umewakusanya mahala na aliyewakusanya ndio mwenye jukumu la kulinda usalama wao pamoja na
"Unapotoa maneno yanayoweza kusababisha muhemko na watu wakakimbizana na kuumia , unawajibu wa kuwajibishwa katika kosa hilo."Nitoe rai kwa viongozi wa madhehebu na shughuli za kidini na mikusanyako mbalimbali wanaowajibu wa kuhakikisha usalama wa watu hao.

"Muchungaji au Mtume Boniphace Mwamposa baada ya tukio hili alitaka kukimbia lakini hivi ninavyozungumza yuko mikononi mwa polisi, na sasa tunafikiria kumtoa Dar es Salaam na kumrudisha Kilimanjaro na kweli yeye wenzake wamesababisha vifo hivyo,"amesema Waziri Simbachawene.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi George Simbachawene


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2RTpDF3
via
logoblog

Thanks for reading WAZIRI MAMBO YA NDANI ATOA KAULI VIFO VYA WATU 20, ATHIBITISHA JESHI LA POLISI KUMSHIKILIA MCHUNGAJI MWAMPOSA..

Previous
« Prev Post