Waziri Kigwangala Azindua Bodi Mpya ya Tanapa

  Masama Blog      

Waziri wa Maliasili na Utalii Hamis Kigwangwala akimkabidhi vitendea kazi mwenyekiti wa Bodi hiyo Generali Mstaafu George Waitara mara baada ya uzinduzi wa Bodi hiyo.
Waziri wa maliasili na Utalii Hamisi Kigwangwala akikabidhi vitendea kazi kwa Katibu wa Bodi mpya ya TANAPA Kamishna wa Uhifadhi Dkt.Allan Kijazi
Picha ya pamoja ya Bodi Mpya ya Tanapa
Waziri wa Maliasili na Utalii Hamisi Kigwangala akikagua Gwaride lililoandaliwa na TANAPA


Na .Vero Ignatus Arusha.


Waziri wa Maliasili na Utalii Dr.,Hamis Kigwangala amezindua bodi mpya ya Tanapa iliyoongezewa muda wake na Raisi John Pombe Magufuli baada ya kumaliza miaka 3 ili iweze kutekeleza majukumu yake ya kuisimamia Tanapa na kuhakikisha utalii endelevu kwa maslahi mapana ya taifa.

Kigwangala ameipongeza wajumbe wa Bodi hiyo kwa kuteuliwa na kuaminiwa na Raisi Magufuli katika kusimamia bodi hiyo ambayo imepewa jukumu la kusimimia Tanapa kwa kipindi kingine cha miaka 3 baada ya kufanya vizuri.

Ameitaka bodi hiyo kuja na mikakati ya kuongeza idadi ya watalii wa nje na watalii wa ndani pamoja na kuhakikisha utalii wa endelevu na shirikishi kwa jamii zinazozunguka hifadhi.

Aidha ameitaka bodi hiyo kutatua migogoro baina ya hifadhi na wananchi ili kuhakikisha kunakua na utalii endelevu ambao ni matunda ya ushirikishwaji wa jamii zinazozunguka hifadhi

Pia ameagiza bodi hiyo kuhakikisha zoezi la uwekaji wa mipaka katika hifadhi unafanyika ili kulinda maeneo ya hifadhi yasivamiwe na kuathiri shughuli za uhifadhi.

Mwenyekiti wa Bodi hiyo Jenerali Mstaafu George Waitara amesema kuwa kwa kipindi cha miaka mitatu bodi hiyo ilifanikiwa kuanzisha jeshi usu,kupambana na ujangili pamoja na kusimamia uhifadhi endelevu kwa maslahi ya taifa.

Kamishna wa Uhifadhi Tanapa ,Dr.Allan Kijazi amesema kuwa wataendelea kushirikiana na bodi hiyo katika kuimarisha na kuendeleza utendaji kazi bora wa Tanapa na hifadhi zilizoko chini yake pamoja na kuongeza mapato yanayotokana na utalii.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2vfgvSg
via
logoblog

Thanks for reading Waziri Kigwangala Azindua Bodi Mpya ya Tanapa

Previous
« Prev Post