WAUZAJI WA VYAKULA KWENYE MIGAHAWA WATAKIWA KUZINGATIA USAFI

  Masama Blog      


 Mtengenezaji wa Juisi katika Mgahawa wa Henry, Wilayani Bukombe, akijieleza mbele ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Zainab Chaula jinsi wanavyoandaa juisi hizo.
Katibu Mkuu Dkt. Zainab Chaula akitoa pesa kuwanunulia juice wauzaji wa mgahawa huo.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Zainab Chaula akikagua usafi kwenye mgahawa huo.
Wauzaji wa mgahawa wakikinga juice waliyonunuliwa na katibu mkuu Dkt. Chaula.
*********************************
Na. Catherine Sungura-Kahama.

Wafanyabiashara wa vyakula na vinywaji nchini wametakiwa kuzingatia usafi wa mazingira wakati wa uandaaji wa bidhaa hizo.

Rai hiyo ilitolewa hivi karibuni na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto – Idara Kuu ya Afya, Dk. Zainab Chaula alipozungumza wafanyabiashara kwenye Mgahawa wa Henry, Wilaya ya Bukombe, Kijiji cha Ushirombo, mkoani hapa.

“Mnatakiwa kuzingatia usafi wa vifaa mnavyotengenezea vyakula pamoja na mazingira yanayowazunguka kwani bidhaa zenu zinatumiwa na watu wengi wa makundi na rika mbalimbali,naona mmeweka grasi chini eneo ambalo kwa kulitazama tu si safi”.Alisisitiza Dkt. Chaula

“Mlipo hapa ni barabarani,kuna vumbi na hamjafunika vyakula vyenu ni rahisi watu kupata magonjwa ya mlipuko kama kuhara na kipindupindu endapo yatatokea,hata wajasiriamali waliopo kwenye maeneo mengine ni vema wakazingatia usafi ili kulinda afya za walaji, kuwaepusha na magonjwa ya mlipuko”.Alisema.

Naye mtengenezaji wa Juisi katika Mgahawa huo, Anneth Ngasa alimhaidi Katibu Mkuu huyo kwamba watahakikisha wanatekeleza yale yote aliyowaagiza kwa mustakabari wa kuwalinda wateja wao.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/39OhGH5
via
logoblog

Thanks for reading WAUZAJI WA VYAKULA KWENYE MIGAHAWA WATAKIWA KUZINGATIA USAFI

Previous
« Prev Post