WATU 20 WADAIWA KUFARIKI DUNIA WAKIGOMBEA KUKANYAGA MAFUTA YA UPAKO

  Masama Blog      
#Moshi: Watu wanaokadiliwa kufikia 20 wanadaiwa kufariki dunia mjini Moshi wakati wakigombea kukanyaga mafuta ya upako yatolewayo na Mtume Boniface Mwamposa katika kongamano linalofanyika uwanja wa Majengo.

Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na Usalama na Mkuu wa wilaya ya Moshi Kippi Warioba amethibitisha kutokea kwa tukio hilo majira ya saa 5:00 za usiku na kwamba hizo ni taarifa za awali.

"Taarifa za awali tulizonazo ni kuwa ni waumini 20 wamepoteza maisha lakini tunaendelea kufuatilia maeneo ya zahanati,vituo vya afya na hospitali kama Kuna watu walipelekewa huko" amesema Warioba.

Idadi ya waliokufa huenda ikaongezeka kwa kuwa hakuna taarifa ya ujumla ya majeruhi waliopelekwa katika vituo vya afya vya jirani pamoja na hospitali ya Rufaa ya KCMC.

Miili ya marehemu imehifadhiwa hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kilimanjaro , Mawenzi.

Tunaendelea kukuleta taarifa hii.....


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/37Qtwjz
via
logoblog

Thanks for reading WATU 20 WADAIWA KUFARIKI DUNIA WAKIGOMBEA KUKANYAGA MAFUTA YA UPAKO

Previous
« Prev Post