Wajasiriamali Watakiwa Kuboresha Vifungashio

  Masama Blog      


Na Woinde Shizza ,Arusha.

Wajasiriamali wilayani Monduli mkoani Arusha wametakiwa kuboresha vifungashio pamoja na ubora wa bidhaa zao ili ziweze kupata masoko ya ndani na nje ya nchi.

Akizungumza katika Maonesho ya Ubunifu,Ujasiriamali na viwanda vidogo  yaliyoandaliwa na shirika lisilokua la kiserikali la Okoa New Generation ,Afisa Mipango wa Wilaya ya Monduli Colex Mwakyelu alisema kuwa wajasiriamali wakiboresha bidhaa zao wanaweza kupata masoko ya nje na kuepuka utegemezi wa masoko ya ndani.

Aliwataka wajasiriamali kuboresha vifungashio na kuzitangaza bidhaa zao katika maonyesho makubwa yanayofanyika ili kupata fursa za masoko na kunufaika kiuchumi.

Mkurugenzi wa shirika lisilokua la kiserikali la Okoa new Generation ,Neema Robert amesema kuwa maonyesho hayo yanalenga kuwapatia fursa za kimasoko pamoja na mafunzo ya wajasiriamali ambayo wamekua wakiyatoa katika majukwaa ya vijana yaliyoko katika wilaya hiyo.

Neema aliwataka vijana kutumia fursa zinazowazunguka kubadilisha maisha yao kwa kuwa wathubutu na wabunifu ili waweze kufanikiwa kiuchumi .

"Vijana wanapaswa kujitoa kufanya shughuli za kujitolea na uzalishaji Mali badala ya kusubiri ajira wakati wanaweza kutengeneza fursa kwa kuamua kujitolea kwanza" Alisema Neema

Kwa upande wake Mmoja wa washiriki wa maonyesho hayo Neema Saidi alisema kuwa kupitia maonyesho hayo yamekua fursa ya kupata wateja na kujifunza kupitia wafanyabiashara wengine juu ya ubunifu na uboreshaji wa bidhaa.

Mjasiriamali Neema Saidi (wapili kushoto) akielezea moja kati ya bidhaa za mavazi wanazozibuni katika maonnyesho ya Ubunifu,Ujasiriamali na Viwanda vidogo yaliyofanyika katika viwanja vya polisi Monduli ,wakwanza kulia ni Mkurugenzi wa Shirika la Okoa New Generation,Neema Robert na wapili kulia ni Afisa Mipango wa wilaya ya Monduli Colex Mwakyelu.Picha na Woinde shizza


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2ukPPiZ
via
logoblog

Thanks for reading Wajasiriamali Watakiwa Kuboresha Vifungashio

Previous
« Prev Post