VIONGOZI WA VYAMA 11 VYA SIASA NCHINI WAMTOLEA UVIVU ZITTO KABWE, WAMLAANI KWA KITENDO CHAKE CHA KUICHONGEA TANZANIA BENKI YA DUNIA ISIPEWE FEDHA

  Masama Blog      
VYAMA siasa 11 nchini vimelaani kitendo cha Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe ambaye pia ni Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo kwenda kuiochongea Tanzania kwa Benki ya Dunia isipate mkopo wa Dola milioni 500 kwa ajili ya maendeleo ya elimu nchini.

Wamesema kitendo hicho kinapaswa kulaaniwa na kila Mtanzania mwenye mpenzi mema na nchi ya Tanzania na kwamba vyama hivyo vina imani fedha hizo zitapatikana na kwenda kusaidia sekta ya elimu na hasa mkakati wa kukabiliana na changamoto ya kukabiliana na mimba mashuleni na hatimaye kuhakikisha mtoto wa kike anapata elimu.

Wakizungumza jijini Dar es Salaam viongozi hao wa Vyama vya siasa 11 wamesema ni jambo la kusikitisha, kuna wanasiasa na Watanzania wanashangilia Tanzania kunyimwa fedha hizo na kwamba mtu wa aina hiyo ni wa kumuonea huruma.

Akizungumza wakati wa mkutano huo Katibu Mkuu wa Democratic Party (DP) Abdul Mluya amesema kwamba hizo fedha ambazo Serikali inazihitaji ni kwa ajili ya elimu na sote tunafahamu elimu ndio msingi wa maisha.
"Sisi tumejaribu kuangalia nani anaathirika kwa kukosekana kwa fedha hizi,  ndugu waandishi wa habari na Watanzania kwa ujumla tukienda kwenye mashule ambako wabunge wetu wanatoka kule mkoani,mashule yale ya msingi na sekondari unaweza usikute hata mbunge mmoja anasomesha mtoto wake katika shule za Kata au kwenye jimbo lake, maana ana uwezo wa kumpeleka mtoto nje ya Tanzania iwe Uganda au sehemu yoyote Duniani na kwenda  kumsomesha na hiyondio tafasiri yake.

"Kwa sisi je ambao hatuna uwezo wa kupeleka watoto wetu Uganda ,International School tutaanyaje,tafsiri yake ni kwamba kugomeshwa kwa hizi fedha au  kuchongea fedha isipate ni kuwakomoa walalahoi ili watoto wao wasisome, lakini kwanini mwaka 2020 ndio watu watu wanatoka ,tafsiri yake watu wanakwenda kuuza nchi, mwaka wa uchaguzi, watu wanakwenda kuuza nchi wapate vipande 30 kwa maslahi yao binafsi na nchi waiingize kwenye shimo," amesema.

Amesema wanasiasa hao wanaokimbilia nje ya Tanzania na kwenda kulalamika na kuiochongea nchi ni vema wakarudi nyumbani ili kuja kuendeleza msuguano ndani badala ya kuuendeleza huko waliko."Kwanza kwanini  hawakwenda mwaka jana, kwanini hawakwenda mwaka juzi.Tulikuwa tunasuguana ndani ,warudi, tuje tusuguane ndani ya mipaka yetu, tusimane na kupigazana kelele tukiwa ndani na hatimaye yote ambayo tunayadai yatapatikana."

Kwa upande wake Mwakilishi wa Chama cha NRA  Hassan Kisabya amesema kwanza anaamini  benki ya dunia hawajazuia kutoa fedha hizo ila anadhani wamechelewesha , kwa hiyo vyama hivyo wanatoa fursa kwa Benki ya Dunia kwani watapima na kupata ukweli.

"Mimi kwenye suala hili nilitaka niseme mambo machache kuhusu namna linavyoweza kutuathiri kama Taifa,kwani huo mkopo wa fedha wa dola milioni 500 ni kwa wanafunzi waliopata ujauzito pekee? Nikajaribu kuangali na kumbe ilikuwa fedha kwa ajili ya maendeleo ya elimu na elimu sio jambo dogo na wala si jambo tu la watoto waliopata mimba bali ni kusaidia mambo mengine ya elimu yetu nchini.

" Fedha hizo zikipatikana huenda zikasaidia kuongezwa walimu,huenda pesa  ile ingesaidia kuongeza miundombinu ya elimu kwa maana ya Maabara na mabweni ,majengo ya madarasa,madawati na vitu vingine.Pia  tukaona katika suala hilo la elimu inaweza kusaidia hata watu wenye ulemavu ambao ni watu wenye haki ya msingi  na wakati mwingine ni maalum kuliko hata hao waliopata ujauzito, kwa mfano kuna QT ambao watu wenye uhitaji maalum wangeweza kutumia nafasi hiyo kupata elimu,"amesema.

Hivyo amewaaambia Watanzania wasikubali kupewa mawazo ya mtu kutokana na itikadi au mlengo wa sera ya Chama chake na ukaathiri Taifa, na kwamba walichobaini tatizo ni muingiliano wa sera kati ya Chama kimoja na Chama kingine au fiikra kati ya mtu mmoja na mtu mwingine .

"Hivyo maoni yetu ni kwamba kwa kuwa mkopo huu ni wa elimu ungegusa watu wote , na wenzetu wanaokwenda kupinga huko watoto wasio miongoni mwa watoto wanaosoma katika shule za watu masikini, kwa hiyo tunalaani Kitendo hichi na kama mwenzetu ana njia nyingine ya kushawishi,atafute utaratibu mwingine na sio kuwafanya wengi waumie kwa kosa la watu wachache sita au saba na kusababisha taifa nzima kuumia. Tunawapinga waliokwenda kuiochongea nchi yetu, na tunawalaani,"amesema.

Wakati huo huo Katibu Mkuu UDP Saumu Rashid amesema Serikali ya Awamu ya Tano imefanya kazi kubwa katika kulinda hadhi ya mtoto wa kike, Serikali imeboresha mifumo ya miundombinu kwa mtoto wa kike kuhakikisha anapata elimu, na sisi kama kama Watanzania kesho au keshokutwa tuwe na viongozi wengi wanawake na lengo ambalo lipo kwenye malengo ya endelevu ya dunia .

"Serikali imeweka kipaumbele katika kuhakikisha usawa wa kijinsia unafikiwa kuwa na wanawake wengi ambao hawatakuwa na ubaguzi katika suala la elimu na ndivyo ambavyo tunaona. Sasa sisi wanasiasa kutumia nafasi yetu ya uanasiasa kuleta majengu au sintofahamu kwa kweli ni suala ambalo kama Watanzania inabidi tulilaani na kulikemea.

"Lakini mwito wangu mkubwa kwa jamii yetu turudishe majukumu yetu ya kuwalea hawa watoto wa kike, tutasema katika nchi mbalimbali kuichafua Tanzania yetu lakini kama hatutaweka jitihada ya kuwalinda watoto wetu wa kike wasipate mimba zisizotarajia kwa ukweli kabisa hatutafikia ndoto yetu ya Tanzania yenye maendeleo ,hivyo turudishe jukumu la kulinda mtoto wa kike,"Hivyo katika mambo ambayo wataangalia, basi wajiangalie hata nini Serikali imefanya katika kumuendeleza huyu mtoto wa kike  ikiwa pamoja na kuhakikisha anakuwa salama kwa kutopata mimba zisizotarajiwa, Serikali imeweka adhabu kubwa ya miaka 30 jela kwa atakayebainika kumpa mimba mwanafunzi.Hivyo  wahusika kwa maana ya benki ya dunia waangalie  ambayo yamefanywa na Serikali na sio kuangalia upande mmoja,"amesisitiza.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa TLP  Richard Lyimo amesema anamuonea huruma Rais Dk.John Magufuli kwasababu yeye anawasaidia Watanzania lakini kuna watu mmpaka leo hawajamuelewa ,kwa hiyo nawaomba wanasiasa mtafute njia nzuri ya kuendeleza Demokrasia ya nchi yetu yetu, lakini pia kuhakikisha amani inakuwepo katika nchi yetu.
 Katibu Mkuu wa Democratic Party (DP)Abdul Mluya akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani),akieleza kuhusu VYAMA vya siasa 11 nchini kulaani kitendo cha Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe ambaye pia ni Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo kwenda kuiochongea Tanzania kwa Benki ya Dunia isipate mkopo wa Dola milioni 500 kwa ajili ya maendeleo ya elimu nchini,Kulia ni Katibu Mkuuwa chama cha NRA,Hassan Kisabya na Kushoto ni Katibu Mkuu wa chama cha  TLP,Richard Lyimo.
 Katibu Mkuu wa chama cha UDP,Saumu Rashid akizungumza
 MKutano ukiendelea
Katibu Mkuu wa chama cha  TLP,Richard Lyimo akifafanua jambo mbele ya Waandishi wa Habari (hawapo pichani),wakati wa mkutano huo


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2vUMnMi
via
logoblog

Thanks for reading VIONGOZI WA VYAMA 11 VYA SIASA NCHINI WAMTOLEA UVIVU ZITTO KABWE, WAMLAANI KWA KITENDO CHAKE CHA KUICHONGEA TANZANIA BENKI YA DUNIA ISIPEWE FEDHA

Previous
« Prev Post