UINGEREZA YAJIONDOA RASMI UMOJA WA ULAYA (EU)

  Masama Blog      

Na Leandra Gabriel, Michuzi TV

UINGEREZA imejiondoa rasmi katika Muungano wa nchi za Ulaya (EU) na kuwa nchi ya kwanza kujiondoa katika umoja huo ambao umedumu kwa miaka 47 kabla ya kuamua kujiondoa kupitia mchakato wa kura za maoni .

Waziri mkuu wa Uingereza Boris Johnson alitangaza mwanzo mpya kwa Uingereza kabla ya kujiondoa.

Kujiondoa kwa Uingereza (brexit)ambako kumeelezwa kuwa ni jambo la kihistoria kumefanyika usiku kwa saa sita kwa saa za Uingereza ambapo maandamano na shangwe vimeelezwa kukafanyika kwa baadhi ya maeneo ambayo yalipiga kura ya kuruhusu kujiondoa.

Waziri Boris ameahidi kuleta nchi hiyo pamoja na kulipeleka taifa hilo mbele zaidi.

Baada ya Uingereza kujiondoa katika umoja huo raia nchini humo  watashuhudia mabadiliko machache yanayoanza moja kwa moja baada ya  nchi hiyo kujiondoa kwenye Muungano wa Ulaya.

Licha ya sheria nyingi za Ulaya kuendelea kuwepo ikiwa ni pamoja na usafiri huru wa raia  hadi Desemba 31 mwaka huu ambapo kipindi cha mpito kitakuwa kinafikia ukomo.

Licha ya kujiondoa katika umoja huo Uingereza inalenga kutia saini makubaliano ya biashara huru na Umoja wa Ulaya, wenye kufanana na ule wa Muungano wa Ulaya na Canada.

Wachambuzi wa mambo kutoka nchi za Ulaya wamenukuliwa wakisema kuwa  Uingereza itapitia wakati mgumu  kufikia makubalino ndani ya siku ya ukomo iliyowekwa.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/36LGttG
via
logoblog

Thanks for reading UINGEREZA YAJIONDOA RASMI UMOJA WA ULAYA (EU)

Previous
« Prev Post